Big idea: Zao la Mpunga ni Biashara yenye mamilioni ya pesa - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 19 December 2016

Big idea: Zao la Mpunga ni Biashara yenye mamilioni ya pesa

Biashara ya Nafaka ni biashara ambayo inalipa na faida yake ni kubwa maana ni lazima utauza na watu ni wengi wanahitaji kinachotakiwa hapa ni utarget aina gani ya zao unalotaka kufanya..
kwa leo nitapenda niongelee zao la mpunga kama zao la biashara kwa mtu alo na uwezo wa kuwekeza na akapata faida nyingi sana...

MTAJI..

Mtaji wa mpunga kwa kununua mkoani morogoro wilaya ya mvomero na kwinginepo tuanzie na milioni 50 ambapo ukienda Mvomero turiani kule wakati wa kuvuna huwa wanauza Gunia moja ni Tsh 60000.
kwa milioni 50 tulizotenga utapata gunia 833 lets say 750 as hapo kuna kupakia mzigo na kushusha then kuna kukodi magari
huu mzigo kwa muda ule ukienda uza soko la dar es salaama gunia kwa wakati huo huwa 80-90 ambapo tufanye ni 85 utapata Tsh milion 63750000 ambapo faida ni zaid ya milioni 13.
hapo ni mahesabu kwa anayezungusha maana yake hapo utaenda fata mzigo tena na tena..
pia kuna sehemu wanalima panaitwa malinyi kule gunia huwa mpaka 40000 ambapo kwa milioni zetu hamsini tungepata gunia 1250 lets make 1100 hizi nyingine tuweke gharama za usafiri utakuja pata milioni 93500000 ambapo faida ni zaid ya milion 40.
sasa hayo mahesabu ni kwa wale wanaozungusha mradi(wananunua na kuuza) ukiamua kuweka ndani na kusubiri bei ipande mpaka gunia kufika laki na 20 (ingawa hufika hadi laki na nusu) kwa gunia 1100 tungepata Tsh milioni 132 (132000000) na hii bei huchukua miezi minne mpaka mitano kufika ambapo huvuna mwez wa 4-6 na kufikia laki na 20 mwezi wa kumi

kwanini nimelichagua zao hili kama wazo kubwa la bishara...?

kwa sababu ubwabwa(wali) ni chakula kinachopendwa sana na watu wa rika zote,jamii zote na hata kiimani watu wote wanakula hili zao...
kwa hiyo ni biashara ya uhakika kwa wenye pesa wakiwekeza katika kilimo,
kikubwa ni kufatilia

Changamoto zake.
kila biashara ina changamoto zake, na hata mpunga una changamoto zake kama hizi hapa chini

1/ Ukusanyaji wa mzigo unahitaji umakini na utulivu usije punjwa ujazo.
2/Muda utakaotumia kukusanya (utahitaji kujitawanya zaid) upate mzigo kwa muda mfupi.
3/location nyingi za kilimo hichi ni vijiji ambavyo vina maji sana kwa hiyo swala la tope kukwamisha gari ni kawaida lazima hilo ulijue pia.
4/lazima ujue target yako katika soko ni lipi na uwingi wa uhitaji wa hilo zao.
namengine mengi utafatilia.

Mwisho

kama unaweza ni vizuri pia ukilima mwenyewe zao hili utapata pesa nyingi zaid ya hizo hapo juu.
na kama hukupata kusoma kilimo cha mpunga unaweza bofya hapa ukaweza kusoma..

Karibu kwa swali,maoni na changamoto pia.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here