Mpunga zao muhimu lenye gharama nafuu - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 11 December 2016

Mpunga zao muhimu lenye gharama nafuu

 
Mpunga ni zao la nafaka ambalo wananchi wengi hulitumia na kutegemea kwa ajili ya chakula. Zao la mpunga linashika nafasi ya pili kwenye mazao ya chakula baada ya mahindi.
Zao la mpunga nchini Tanzania linalimwa zaidi katika mikoa ya Morogoro, Arusha, Shinyanga, Tanga, Mwanza Tabora, Mbeya, Rukwa, Manyara, Iringa na Kigoma.
Wananchi walio wengi hutumia kwa ajili ya chakula hasa nyakati za usiku. Kutokana na mahitaji yake kuwa makubwa hasa kutokana na ongezeko la watu, uzalishaji wa mpunga nao  umekuwa ukiongezeka siku hadi siku.Hivi sasa, nchi ya Tanzania ina eneo la uzalishaji wa mpunga lipatalo hekta 854 000 ambapo uzalishaji ni zaidi ya tani 2,213,020 kwa msimu.

Uzalishaji
 
Zao la mpunga linastawi kwenye eneo lenye udongo wa mfinyanzi (udongo unaotuamisha maji). Eneo hilo ni lazima pia liwe na maji mengi kwa kuwa zao hili linahitaji kiasi kikubwa
cha maji ili kustawi.Zao hili ni rahisi kuzalisha kwa kuwa halihitaji mbolea nyingi kama ilivyo kwa aina nyingine za mazao, halikadhalika hakuna magonjwa mengi  yanayoshambulia zao la mpunga.

Aina za mpunga

Kuna aina nyingi za mpunga ila baadhi miongoni mwa zinazofanya vizuri ni pamoja na Super, Karamata, Kahogo, na Saro.

Matumizi:

Hili ni zao la chakula, na pia ni zao la biashara, ambapo kuna aina nyingi ya bidhaa zinazoweza kutengenezwa kutokana na zao hili.

Namna ya kupanda

Kuna aina mbili za upandaji wa mpunga.

mbegu shambani

Mbinu hii hurahisisha nguvu kazi. Hata hivyo mbinu hii ina hasara zake kama vile kiwango cha mbegu zinazoota, na pia uwepo wa magugu mengi katika eneo husika.

panda kwa mstari.

Hii ni aiana nzuri zaidi na inayopendekezwa kitaalamu, ambapo mbegu hupandwa kwenye kitalu na kisha baadae hupandwa shambani kwenye shamba lililoandaliwa baada ya wiki 3 mpaka 4, kulingana na mwanga wa jua, joto na aina.

Kuandaa shamba la mpunga
 
Umwagiliaji

Maandalizi ya shamba huanza kwa kumwagilia kwanza sehemu ya shamba mpunga utakapopandwa, maji yajae kiasi cha sentimita 10 kisha lilimwe. Inashauriwa kuwa shamba lilimwe na kisha kunyeshewa tena walau siku 15 kabla ya kupanda.

Nafasi

Nafasi hutegemeana na aina ya mpunga. Mfano, mpunga aina ya “Basmati 217” inapasa kupandwa kwa nafasi ya sentimita 20x10. Aina nyinginezo zinaweza kuwa 20x20.
Inashauriwa kupanda kwa mistari kwa kuwa upandaji wa aina hii ndiyo wenye matokeo mazuri kiuzalishaji, na hurahisisha kazi hata wakati wa palizi.

Muda

Zao hili huchukua muda wa miezi 5  6 tangu kupandwa hadi kuvuna.

Uvunaji

Kwa heka moja ya mpunga inakadiriwa kupata gunia 1530 ambapo kwa mauzo ya kila gunia tsh 80000 utapata tsh 1200000 mpaka 2400000 ambapo katika heka moja gharama ya ulimaji inafikia laki tano.
Ni faida nzuri sana ni kuamua na kutekeleza dhima yako

Uhifadhi

Mpunga unaweza kuwekwa kwenye magunia na kuhifadhiwa stoo kwa muda mrefu bila kuwekwa dawa, hii ni kwa sababu wadudu wanaoshambulia mpunga sio wengi.

Soko

Mchele wa Tanzania una soko zuri la ndani na nje ya nchi, jambo linalofanya uzalishaji pia uongezeke. Kasi ya ongezeko la watu hapa nchini pia ni kichocheo cha ukuaji wa soko kuto kana na uhitaji wa zao hili.

Changamoto

Tatizo kubwa linalokabili zao hili nchini Tanzania ni uhaba wa ardhi ya kutosha inayotosheleza uzalishaji wa zao hili kwa wingi. Hii inatokana na maeneo mengi kutumiwa na wakulima na wafugaji.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here