Kilimo mseto huongeza uzalishaji wa mazao, malisho na utunzaji wa mazingira - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 11 December 2016

Kilimo mseto huongeza uzalishaji wa mazao, malisho na utunzaji wa mazingiraMara nyingi wafugaji wa mbuzi na wanyama wengine huendesha shu-ghuli za kilimo, katika mashamba yao kwa kuotesha mimea ya aina mbali mbali. Hii ni pamoja na miti malisho.


Kilimo mseto ni mfumo wa kilimo wa kuchanganya miti na mazao katika shamba moja. Miti sahihi kwa kilimo mseto humnufaisha mfugaji kwa njia nyingi. Miti hiyo huweza kutumiwa  kama malisho ya mifugo. Baadhi ya miti hutoa matunda mazuri kwa matu-mizi ya binadamu. Zaidi ya hayo, kilimo mseto huzuia mmomonyoko wa udongo na kurutubisha ardhi. Kadhalika kilimo mseto hudumisha rutuba iliyoko kwenye udongo.

Kuzuia mmomonyoko wa udongo

Miti huimarisha zaidi makingo ya maji katika shamba na kuzuia mmomonyoko wa udongo kwa namna ifuat-avyo;
 
v  Kupunguza kasi ya maji, kufanya maji yaingie kwa wingi kwenye ardhi na hivyo kupunguza maji yatembeayo juu ya shamba.
v  Kupunguza kasi ya upepo, hivyo kupunguza uwezo wa upepo kuchukua udongo.
v  Kunasa udongo uliochukuliwa na maji au upepo.
v  Kuongeza mfuniko wa ardhi kuto-kana na matawi na majani yaangu-kayo, hivyo kupunguza uwezo wa matone ya mvua kuanzisha mmomon-yoko wa udongo.
v  Kusababisha kutokea kwa ngazi (terrace) kutokana na kukusanyika kwa udongo toka sehemu ya juu ya shamba.
v  Kuimarisha umbile la udongo kutokana na mboji inayojitengeneza na majani yanayoanguka. Hali hii huufanya udongo uwe na uwezo wa kuhimili nguvu za maji na upepo ili zisiweze kuanzisha mmomonyoko wa udongo.
v  Kurutubisha na kudumisha rutuba ya udongo.Kutokana na kuzuiliwa kwa udongo, rutuba itadumu kwa muda mrefu zaidi kwani kutakuwa hakuna upotevu.
v  Miti mingi itumikayo kwa kilimo mseto ina uwezo wa kuchukua kirutubisho cha aina ya naitrojeni kutoka hewani na kukitunza kwenye mizizi, mashina na majani. Majani yaangukayo shambani na kuoza huongeza katika udongo kirutubisho hiki muhimu kwa  mazao.
v  Kadhalika baadhi ya miti huweza kuwa na mizizi mirefu inayopenya kwa kina kirefu ardhini na kufyonza virutubisho kutoka chini sana kwenye  udongo, eneo ambalo mizizi ya mazao  mengi ya kawaida haiwezi kufika. Kwa kufanya hivyo, miti hiyo huleta viru-tubisho hivyo juu na kuviweka kwenye sehemu za mmea wenyewe kama vile majani. Mara majani hayo yanapoan-guka ardhini na kuoza, virutubisho hivyo hubaki kwenye udongo lakini sasa katika kina kinachoweza kufikiwa na mizizi ya mazao ya kawaida.
v  Mboji itokanayona kuoza kwa majani yaliyoanguka huongeza uwezo wa udongo kushikilia virutubisho bila kuviachia viyeyushwe na maji na kupenya chini zaidi kwenye kina kirefu ambacho hakitaweza kufikiwa na mizizi ya mazao na hivyo kupotea bure. Pia, mboji husaidia kudumisha unyevu kwenye udongo.
v  Kutokana na uwezo wa miti kurutubisha na kudumisha rutuba ya udongo, matumizi ya mbolea ya chumvichumvi yatapungua sana na hayatakuwepo kabisa. Kwa kuwa hakutakuwa na haja ya kununua mbolea za aina hiyo gharama za uza-lishaji wa mazao zitapungua.Kutoa malisho ya mifugo Miti ya kilimo mseto kama vile lukina hutumika kwa malisho ya mifugo kama mbuzi, ng’ombe na kondoo. Wafugaji wadogo wa mbuzi wanaweza kutumia matawi, majani, vikonyo, matunda au mbegu za miti kuongeza malisho ya wanyama wao.Wakati mwingi wa kiangazi chakula cha wanyama huwa haba wakati ambapo miti huendelea kutoa malisho.

Faida zitokanazo na miti ya kilimo mseto
 
v  Miti iliyopandwa na kuachwa kure-fuka hutoa kivuli ambacho huburudi-sha wanadamu pamoja na mifugo pia.
v  Miti huweza kumpatia mkulima kuni.
v  Miti itumikapo kama kuni hum-punguzia mkulima umbali na muda ambao angeutumia kutafuta kuni.
v  Miti ni kinga au akiba kwa mkulima na anaweza kuiuza au kutumia wakati wa matatizo ya kiuchumi.
v  Mazao ya miti yanawezakum-wongezea mkulima kipato.Miti ya matunda inapotumika kwa
v  kilimo mseto, hutoa matunda kama maparachichi, mapera, maembe na mac-hungwa ambayo ni sehemu muhimu kwa lishe ya binadamu.
v  Miti hutoa vifaa vya ujenzi kama mbao, fito na nguzo.
v  Miti hufanya mazingira ya shamba na nyumba za wakulima kupendeza na kuvutia zaidi.
v  Miti huweza kuvuta nyuki ambao wakiwekewa mizinga wataweza kuzali-sha asali.

Madhara ya kilimo mseto kama hakitaendeshwa vizuri

Kama masharti ya kilimo mseto hayata-fuatwa kama inavyotakiwa, madhara kadha huweza kutokea.

Kwa mfano

v  inashauriwa kuwa matawi ya miti ya kilimo mseto yapunguzwe mara kwa mara. Ikiwa hayatapunguzwa vizuri;
v  Mazao karibu na miti hayatastawi na kuzaa vizuri. Hii ni kwasababu mazao hayo hayatapata mwanga wa kutosha. Vilevile, mazao hayo yatakosa virutubisho pamoja na unyevu wa kutosha kutokana na mahitaji makubwa ya virutubisho na unyevu ya miti yenye matawi mengi.
v  Yanaweza kuwa sehemu ya kujificha ndege, wanyama waharibifu, wadudu au hata magonjwa na kudhuru mazao hapo baadaye.

Aina ya miti inayofaa kwa kilimo mseto

Katika kilimo mseto, si miti yote inafaa kupandwa, miti ya kilimo mseto huwa na sifa maalumu ambapo mkulima anafaa kuchagua miti anayoipenda kutegemeana na mahitaji yake na sifa za miti.

Sifa ya miti ya kilimo mseto

v  Iwe na matumizi ya aina nyingi kama vile kuni, mkaa, nguzo, fito, mbao, madawa na malisho kwa mifugo.
v  Iwe na mizizi inayokwenda chini

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here