Jua tofauti ya groups za utafutaji pesa katika Nyanja tofauti. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 12 December 2016

Jua tofauti ya groups za utafutaji pesa katika Nyanja tofauti.
Inapokuja katika swala la kazi, kuna watu huwa wanakuja na uoga wa kujikwamua katika maswala ya uchumi wakiwa wanalengo la kupata mkataba kama ndio nguzo yao ya maisha. Tukiongelea mshahara(faida) watu wengi wanapenda kupata hadi cha nyongeza kwa sababu ndio lengo kuu la kila mtu.


Hapa chini nimejaribu kuelezea tofauti kati ya ngazi tofauti katika nyaja za utafutaji pesa,ambapo tunaanza na:-

MUAJIRIWA(Employee)

Sasa tukiongelea mwajiriwa ni Yule mtu ambae anaujuzi wa jambo Fulani ambae anakuwa anamfanyia mtu, kampuni au taasisi kazi Fulani then baada ya muda flani analipwa kutoka katika faida aliyoingizia kampuni au taasisi ile. Huyu huwa anapangiwa kazi na muda wa kuwa kazini.
Mtu huyu huwa ni mnyonge na yupo chini ya utawala flani ambao ndio unaoamua kuwepo kwake kazini na malipo yake huku yeye akiwa anapata asilimia ndogo kutokana na faida aloingizia kampuni,taasisi au shirika flani.

KUJIAJIRI (Self-employed)

Hawa ni watu ambao wanataka wao wenyewe kuwa ma boss hawataki kuwe na bosi mwingine juu yao, na wanafanya kazi wenyewe(hawana haja ya kuajiri) hawa mi nawaita (do it yourselfers)
Tukija katika maswala ya pesa huyu mtu hufanya kazi sana ili aweze kuingiza pesa nyingi zaid na hupenda pesa yake isikatwe katika mambo mengine nje ya kazi aloifanya.
Kasoro katika hii nafasi ni kuwa huyu alojiajiri atafanya kazi kila siku za maisha yake, pale atakapo acha kufanya kazi na mapato yake yatasimama kwa maana mapato yake yanamtegemea yeye kujishughulisha zaid

WAMILIKI WA BIASHARA (Business owner)

Tofauti ya hili group na la kujiajiri ni kuwa mtu huyu hutaka kuzungukwa na watu smart,wale wa kweli(waajiriwa), pia kujiajiri mara nyingi hawaamini kama mwingine anaweza fanya kazi yake vizuri kama yeye anavyofanya lakini group hili wao huamini zaid katika kuweka watu wafanye kazi zao na wao wakafanye au kubuni kazi nyingine huku wakiamini mwisho wa mwezi faida inayopatikana atampatia kibarua wake kiasi kidogo na kitakachobakia ni chake
Wanatumia principal ya (KWANINI UFANYE WEWE WAKATI WAPO WATU WATAKAOFANYA VIZURI NA UKAWALIPA KIDOGO)

TOFAUTI YA WAMILIKI NA WALOJIAJIRI

Wamiliki wanaweza kuondoka na kuacha biashara zao miezi au miaka na wakirudi wanakuta biashara yao imepata faida nyingi tu lakini alojiajiri akithubutu kuondoka tu atakaporudi atakuta biashara imesimama ikimsubiri yeye aje aendeleze

Soma Mambo Ya Kuzingatia, Kama Wewe Ni Mjasiriamali Unayetaka Mafanikio Makubwa.


WAWEKEZAJI (Investor)

Muwekezaji anatengeneza pesa kwa kutumia pesa. Hawana haja ya kufanya kazi kwa sababu pesa zao ndio zinafanya kazi kwa ajiri yao.
Hii ndio quadrant inayoleta utajiri, Regardless quadrant gani watu wanatengezea pesa ila I hope someday watafikia hapa kutengeneza utajiri kwa sababu utakuwa na uwezo mkubwa wa kutanua biashara zako zikawa nyingi kwa muda mmoja, ni hatua ya mwisho ambapo pesa ina geuzwa na kuwa utajiri.

Ahsante kwa kuwa nasi, fatilia makal zetu kila siku upate kubadili maisha yako

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here