Jinsi uhusiano wa kimapenzi unavyoweza kuanzishwa bila kutarajiwa - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 21 December 2016

Jinsi uhusiano wa kimapenzi unavyoweza kuanzishwa bila kutarajiwa

 shafiinad.com
Unaweza kushangaa lakini ndio ukweli wenyewe kwamba upo uwezekano mkubwa kabisa wa kuanzisha na kuendeleza mahusiano na mtu yeyote bila kujali mwonekano wake, tabia yake na imani yake. Katika makala haya tunaeleza kanuni za kimaumbile zinazoongoza mahusiano ya watu wawili ambao mara nyingi watu hao hukutana kwa njia ya nasibu.

Pamoja na imani kwamba mahusiano bora huwezekana kwa kukutana na mtu sahihi, tunaambiwa na watalaam wa mahusiano kwamba mwanamke yeyote anaweza kabisa kuwa na mahusiano na mwanaume yeyote kwa amani ikiwa kila mmoja wao atakuwa 'motivated' kujua mahitaji ya mwenzi wake huyo na kuyajibu ipasavyo.

Lakini kabla sijaeleza zaidi, nikumbushie mambo makuu matatu tuliyoyaona katika makala ya nadharia ya mahusiano na mapenzi ambayo ndiyo yanayoanzisha mahusiano kwa maana ya kuwafanya watu wawili wapendane. Mambo hayo ni:

1) Hisia za kimapenzi au tamaa.  Ingawa tamaa ina nguvu kubwa sana katika kuanzisha mahusiano, haiwezi kudumisha uhusiano huo kwa muda mrefu. Misingi ya hisia hizi za kimapenzi ni maumbile yanayoonekana.

2) Urafiki au ukaribu unaojenga mazingira ya watu wawili kuwa karibu kihisia. Tuliona kuwa misingi ya ukaribu huu ni namna gani mahitaji ya kihisia ya mwenzi yanavyotambuliwa na kujibiwa bila kujali urafiki huo umetokana na tamaa au maamuzi na huu ndio msingi wa maamuzi.

3) Maamuzi ya kuweka ahadi. Ingawa kwa wengi dhamira ya kudumisha uhusiano hutokana na mawili ya awali, wakati mwingine, hutokea maamuzi hayo yakawa chanzo cha kuchipua kwa urafiki na hisia kama ilivyokuwa kwa wazee wetu zamani. Hiki ndicho kiwango cha juu cha uhusiano.

Sasa, ingawa uhusiano unaweza kuchipukia kokote kati ya tamaa, urafiki na maamuzi kutegemeana na imani, mitazamo na utamaduni wa wahusika, kilicho muhimu zaidi ni kile kinachofanyika baada ya uhusiano huo kuanzishwa ili kuufanya uendelee. Katika makala hii tutafafanua zaidi conditions muhimu za kuupeleka uhusiano huo mbele kama tulivyoahidi.

Mahusiano yanavyoanza

Kwa kawaida, uhusiano huanza pale mtu anapovutiwa na mwingine iwe kihisia au kimwili. Hiyo ndiyo hatua ya kwanza kabisa ya mahusiano ambayo hutegemea masuala makuu mawili.

Kwanza kabisa, ni ukaribu, propinquity. Tunaambiwa kwamba, watu wawili wanapojikuta bila hata wao wenyewe kutarajia katika mazingira ya ukaribu iwe kwa kufanya pamoja kazi ofisi moja, kuabudu mahali pamoja, kusoma mahali panapofanana au kuishi mtaa mmoja, huongeza uwezekano wa mmoja wao kuvutiwa na mwenzake na hivyo kuanzisha mahusiano.

Tafiti zinathibitisha kwamba kadri unavyokutana na mtu iwe kwa kumwona na kumsikia mara kwa mara, ndivyo unavyoongeza uwezekano wa kumpenda (liking) na kwamba kwa kawaida, hatuvutiwi na vitu tusivyojua kwa karibu ikiwamo watu. Kwa maana nyingine, kadri unavyokutana na mtu ndivyo unavyojikuta ukiongeza evaluation ya kumpenda.

Kwa upande mwingine, ukaribu huu huongeza uwezekano wa kufanana mambo fulani fulani kama imani na mitazamo na hivyo kuongeza ukaribu. Mfano, vijana wanaokutana kanisani mara kwa mara kwenye ibada, mbali na kuongeza uwezekano wa kuvutiana, lakini pia huongeza uwezekano wa watu hao kuwa na imani, mitazamo na interests zinazofanana. Haya matatu huwa ni kichocheo cha mvuto unaojenga mawasiliano ya kimapenzi.Jambo la pili linaloanzisha mahusiano ni mvuto wa kimwili. Hapa tunazungumzia uzuri wa sura, urefu/ufupi, unene/wembamba, weupe/weusi na kadhalika. Sasa, uzuri ni relative.  Watu wanatofautiana namna wanavyotafsiri uzuri kutegemeana na utamaduni, malezi, imani na sababu nyinginezo. Na wakati mwingine, uzuri wa mtu hutegemea pia 'viwezeshi' vingine kama mavazi, mapambo, anavyozungumza, anavyotazama na kadhalika.

Vyovyote vile iwavyo, wengi wetu huamini mtu mwenye mwonekano tunaouona sisi kuwa ni mzuri, basi automatically huwa na haiba na tabia njema. Tuna mazoea ya kuhusianisha uzuri unaoonekana na uzuri usioonekana. Ni aina fulani ya stereotype yenye misingi yake kwenye malezi. Kwamba mzuri ana tabia nzuri jambo ambalo hutufanya tutamani kuhusiana na watu tunaowachukulia kuwa wazuri.

Hata hivyo, tunaambiwa, pamoja na kwamba watu wengi hutamani kujenga mahusiano na watu wenye mwonekano mzuri wa kimwili, mara nyingi huishia kujenga mahusiano na watu wenye mvuto unaolingana na mvuto walionao wao wenyewe. Unajikuta unahusiana na mtu anayefanana na wewe kwa kiasi fulani. Ni hivyo mara nyingi. Ndio kusema, wanaotamani kuhusiana na watu fulani wenye uzuri wa viwango fulani, hujikuta wakihusiana na watu wa kawaida kama wao. 

Bahati mbaya ni kwamba, mwonekano wa mwili huwa na nafasi kubwa katika hatua za mwanzo za uhusiano na kuwa mahusiano ya kudumu huwa hayategemei mvuto kama nitakavyoeleza katika aya chache zinazofuata. Lakini pamoja na matatizo yake, uzuri wa sura na umbo una nafasi yake, kubwa tu, ya kumfanya mtu ajiingize kwenye mahusiano.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here