Zao la karoti linainua pato la wakulima - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 7 November 2016

Zao la karoti linainua pato la wakulimaKaroti ni zao la mizizi ambalo hulimwa zaidi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa, Mbeya na Kagera. Uzalishaji wake ni sawa na wastani wa tani 1735 kwa mwaka kulingana na takwimu za mwaka 2003.
 
Karoti ni mojawapo ya mazao ya jamii ya mbogamboga, zinazotokana na mizizi. Mizizi yake hutumika kama mboga na pia huongeza ladha kwenye mchuzi na aina nyingi ya vyakula.  Mizizi ya karoti iliyosagwa huon-gezwa kwenye saladi na pia hutumika kutengeneza achari pamoja na juisi. Zao la karoti lina madini ambayo ni moja ya kiungo kinachotengeneza vitamini A.

Mambo ya kuzingatia wakati wa uzalishaji Ili kupata karoti nyingi na bora ni muhimu kuzingatia kanuni za kilimo cha karoti.

Baadhi ya kanuni hizo ni kama zifuatazo:

Kuchagua aina ya mbegu

Ni muhimu sana mkulima akachagua aina bora ya mbegu kulingana na matakwa ya soko. Pamoja na mahitaji ya soko, ni muhimu pia kuchagua aina inayovumilia mashambulizi
ya magonjwa na wadudu, kuchagua mbegu inayokomaa mapema na yenye kutoa mazao mengi na bora.Mkulima anaweza kupata mbegu za karoti kutoka katika maduka ya
wauzaji wa mbegu waliothibitishwa au katika mashamba ya wazalishaji wa mbegu wanaotambulika, au kutoka katika vyama vya ushirika.Unaweza kuotesha kiasi cha gramu  150-200 za mbegu kwa kila skwea mita mia moja.

Aina za karoti nchini Tanzania

Flaccor (Flakoro) - Aina hii ya karoti ina mizizi mirefu.

Chacteray redcove - Aina hii ina mizizi. mifupi kiasi.

Oxheart - Aina hii ya karoti ina mizizi mifupi na minene.

Chantenay - Aina hii ya karoti ina mizizi mifupi kiasi.

Hali ya hewa

Karoti inaweza kuzalishwa katika hali za viwandani hakikisha unamuona mtaalamu wa kilimo kwa ushauri.

Kuotesha mbegu

Karoti ni aina ya zao ambalo husiwa moja kwa moja shambani (halipan-dikizwi). Mbegu husiwa moja kwa moja shambani kwa nafasi ya sentimita 41-50 kutoka mstari hadi mstari. Baada ya uotaji wa mbegu, punguza miche iwe na umbali wa sentimita 5 toka mche hadi mche. Upunguzaji ufanyike wakati udongo ukiwa na unyevu wa kutosha ili kutoharibu  miche mingi na kung’oa miche ambayo haikukusudiwa kung’olewa.

Kuota

Mbegu ya karoti huota kati ya siku 10 hadi 15 toka kusiwa na ili kurahisisha uotaji, inashauriwa kuloweka mbegu kwa saa 24, kisha zichanganywe na mchanga tayari kwa kuotesha.

Mpangilio

Zao la karoti hupangiliwa shambani kwa kufuata hatua mbili muhimu:

Hatua ya kwanza

Punguza miche kwa kung’oa mara moja kuondoa miche iliyosongamana.

Hatua ya pili

Punguza tena miche kwa kung’oa pale inapokuwa na urefu wa sentimita 10-15

Utunzaji wa shamba

Palizi:

Palizi ya kutumia jembe la mkono husababisha uharibifu wa mazao kwani karoti mara nyingi hukatwa mbalimbali, ingawa huwa na matokeo mazuri zaidi inapozalishwa sehemu zenye baridi ya wastani. Karoti hustawi zaidi katika mwinuko wa mita 1000 kutoka usawa wa bahari, pamoja na mvua za wastani. Hali ya ubaridi huhitajika sana wakati inapokaribia kuvunwa ili kuweka rangi nzuri na umbo la mizizi yenyewe.

Udongo

Zao la karoti hustawi katika udongo wenye rutuba ya kutosha. Usiweke mbolea ambayo haijaiva vizuri kwenye eneo unalotarajia kupanda karoti kwani husababisha mizizi kuoza na  pia husababisha mizizi kukunjamana, jambo ambalo huathiri uzalishaji.Utayarishaji wa shambaIli kuwa na matokeo mazuri, inashauriwa matayarisho ya shamba yafanyike mapema kabla ya msimu wa upandaji. Ni vizuri udongo ukati-fuliwa vizuri na kuwa laini na kina cha sentimita 30 kwa ajili ya kuotesha karoti.

Mbolea

Haishauriwi kuweka mbolea mbichi (ambayo haijaoza) kwenye shamba linalopandwa karoti. Ni vizuri zaidi kutumia mbolea ya mboji ambayo imeiva vizuri au aina nyingine ya mbolea za asili zisizokuwa na madhara kwa afya ya binadamu na mazingira, na inayoweza kuongezwa kila baada ya mwezi mmoja kama kuna uhitaji. Ni muhimu sana kurutubisha  udongo ili kupata mazao mengi na yenye ubora yanayoweza kuhifadhika vizuri. Ikiwa ni lazima kutumia mbolea

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here