ULIMAJI WA ZAO LA MANANASI - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 10 November 2016

ULIMAJI WA ZAO LA MANANASIMananasi ni matunda yanayolimwa kwa wingi katika
mikoa ya Pwani, Kigoma Morogoro, Tanga,Mwanza na Dar es Salaam. Uzalishaji wake ni wastani wa tani 214,840 kwa mwaka ambayo niasilimia 17.9 ya mazao yote ya matunda. Mananasi ni zao la biashara na chakula.
 
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUZALISHA

Ubora wa mananasi hutegemea jinsi yalivyozalishwa. Hivyo ni muhimu kuzingatia kanuni za kilimo bora cha mananasi wakati wa uzalishaji ili kupata matunda yenye ubora unaotakiwa.

Baadhi ya kanuni za kuzingatia ni kama zifuatazo:

Kuchagua aina bora
• Chagua aina bora ya kupanda kulingana na mahitaji ya walaji na soko.

Kudhibiti magonjwa na wadudu
• Dhibiti magonjwa na wadudu mapema ili kupata mazao bora  yanayoweza kuhifadhiwa na hatimaye kusindikwa kupata bidhaa bora.

Palilia shamba
• Palilia shamba ili kuondoa magugu. Magugu hupunguza rutuba na ubora wa mananasi wakati yanaposhindania virutubishi na mimea. Hakikisha barabara ndani ya shamba ni safi ili kurahisisha uvunaji na usafirishaji wa mananasi.

Kagua shamba
• Fanya ukaguzi wa shamba mara kwa mara ili kugundua madhara ya mashambulizi ya wadudu na magonjwa yanayoweza kujitokeza.

Hakikisha mananasi yamesimama wima na yanapata mwanga wa kutosha katika pandezote ili yawe bora.
­­­­­­­, ­­­­­­­­­­ ­­ ­­­­­­­­ ­­ ­­­­­ ­­ ­­­­­­­ ­­ ­­­­­ ­­
Kudhibiti ukubwa wa mananasi
Mananasi yanayotakiwa kwenye soko ni lazima yafikie viwango vinavyotakiwa na walaji. Hivyo rekebisha ukubwa wa matunda kufuatana na mahitaji ya soko Ilikupata mananasi yenye ukubwa wa kati rekebisha kwa kutumia njia zifuatazo:
• Nyunyizia dawa ya fruitone ambayo hufupisha ukuaji wa vikonyo
• Ondoa majani ya katikati ya kilele (crown) ambayo husababisha ukuaji mara baada ya
ukubwa wa nanasi kufikia kiwango kinachohitajika. Iwapo soko  linahitaji mananasi makubwa ni vyema kuacha majani ya kilele cha ukuaji ili nanasi liendelee kukua hadi kufikia ukubwa unaotakiwa Kuzuia matunda yasibabuliwe na jua.
Mananasi yana tabia ya kuegemea upande. Hali hiyo husababisha upande mmoja wa tunda kubabuliwa na jua. Mananasi yaliyobabuliwa na jua upande mmoja ubora wake hushuka. Ili
kuzuia hali hiyo, zingatia yafuatayo:

• Hakikisha kuwa tunda la nanasi liko wima na linapa
ta mwanga wa kutosha pande zote.

• Kwa mananasi yaliyoegemea upande mmoja jaribu kuyafanya yakae wima kwa kutumia miti yenye pande, kisha funika kwa majani au makaratasi.

Kung’arisha mananasi
Wiki moja kabla ya kuvuna ng’arisha matunda kwa kunyunyizia dawa ya ethephone kiasi chamililita 70 kwa lita 1000 za maji. Dawa hii hufanya matunda yawe na rangi ya kung’ara na kuvutia soko.
 
Matayarisho kabla ya kuvuna

Kukagua shamba kuona kama yamekomaa
• Mananasi hukomaa katika kipindi cha miezi 12 hadi 24 tangu kupanda kutegemea aina yachipukizi zilizopandwa

Dalili za nanasi lililokomaa
Rangi ya tunda hubadilika kutoka kijani na kuwa ya manjano au rangi ya machungwa kutegemea aina.

Majani ya katikati ya kilele hunyofoka kwa urahisi.

Hutoa harufu nzuri ya nanasi lililoiva

Tunda likigongwa na kidole hutoa sauti nzito.

Kwa tunda lililokomaa kipimo cha kupimia kiwango cha
sukari (refractometer) kitaonyesha asilimia isiyopungua 12
 
Kuvuna
Ni muhimu kuvuna mananasi kwa wakati unaotakiwa ili kuepuka upotevu wa mazao. Njia bora ya kuvuna mananasi hapa nchini ni kwa kutumia mikono, ingawa nchi nyingine uvunaji wa mashine hutumika.

Kata mananasi pamoja na kikonyo chake kwa kutumia kisu kikali. Urefu wa kikonyo uwe sentimita 10 kutoka kwenye shingo ya tunda.

Usitumie kisu butu kwa kukata kwani ukataji huo husababisha nanasi kuoza kutokana na kuingia kwa urahisi kwa vimelea vya magonjwa.

Wakati wa kuvuna hakikisha matunda hayakwaruziki,au kuchubuka.

Wakati wa kuvuna mananasi yaweke kivulini ili kuepuka jua ambalo huongeza kasi ya uharibifuwa matunda.

UKIPATACHO
Kwa Uzoefu nilonao kwa ekari moja inagharimu mpaka million moja lakin kama utatumia na nguvu zako hii gharama hupungua mara mbili yake na kumfanya mtu kuweza kulima sehemu kubwa sana na kupata faida kubwa zaid
Kwa heka moja unaweza kuvuna hadi miche 25000 ambayo kila NANASI moja uuze elfu moja hapo ukja toa na gharama utaona kinachobakia…
Siku zote anayewekeza sehemu kubwa ndio hupata faida kubwa…

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here