Ukizingatia kanuni hizi utafanikiwa kuwa na uzalishaji bora wa mazao - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 7 November 2016

Ukizingatia kanuni hizi utafanikiwa kuwa na uzalishaji bora wa mazao1.Usafishaji wa shamba

Shamba likiwa safi unapunguza sehemu ambazo wadudu wanaweza kuzaliana kwa urahisi, pamoja na sehemu ambazo vitu vinavyosababisha magonjwa vinaweza kujificha.
Mkulima anashauriwa kupalilia shamba lake mara kwa mara na kila inapowezekana kuhakikisha anaondoa masalia ya mazao ya msimu uliopita shambani.Masalia hayo yakibaki shambani wadudu wa magonjwa ya mazao hayo vitaendelea kuwepo na kuzidi kuzaliana.


2. Kilimo cha mzunguko

Unapoliama zao la aina moja kwenye eneo moja kwa muda mrefu, magonjwa na wadudu wa zao hilo vitaendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka. Mkulima anapaswa abadilishe mazao
kila msimu. Mazao yatakayopandwa kwenye mzunguko yawe ya jamii tofauti. Hii ina maana kuwa yawe yanashambuliwa na wadudu na magonjwa tofauti na msimu uliopita.

3. Upandaji wa mbegu vumilivu

Kila inapowezekana tumia aina ya mbegu inayostahimili uharibifu wa magonjwa na wadudu(resistance varieties) ambazo hazishambuliwi kwa urahisi.

4. Matumizi ya mbolea ya samadi/mboji

Mkulima anapotumia mbolea ya kutosha kwenye mazao yake mimea inakuwa na nguvu hivyo inastahimili mashambulizi ukilinganisha na mimea ambayo haina mbolea kabisa.

5. Matumizi ya mbegu bora na safi

Wakati wa kuchagua mbegu, mkulima anapaswa kuchagua mbegu kutoka kwenye mimea iliyo bora katika shamba lake. Ukichukua mbegu kutoka kwenye mmea wenye ugonjwa utahamisha ugonjwa huo kutoka eneo moja hadi lingine na hata kutoka msimu mmoja hadi mwingine. Hakikisha kila inapowezekana mbegu zinanunuliwa kutoka kwenye maduka yanayoaminika. Endapo utalazimika kutayarishambegu, hakikisha unazipata kutoka kwenye miche iliyo bora, na yenye afya nzuri. Tofauti na hapo hakikisha unanunua mbegu kutoka kwenye makampuni ya mbegu yaliyosajiliwa.

6. Kupogoa

Kila mkulima anapoona dalili za ugonjwa, ni muhimu kuondoa sehemu yenye ugonjwa kwenye mmea. Kwa mfano, ugonjwa wa ukungu kwenye nyanya. Unapoona dalili za kwanza za ugonjwa huo kwenye jani, basi tahadhari ya kwanza ni kuiondoa sehemu  ya majani yenye ugonjwa ili usienee kwenye majani au mimea mingine.

7. Kutandaza nyasi (Mulching)

Mbali na kuzuia magugu yasiote kwa urahisi, pia matandazo huzuia baadhi ya magonjwa yasishambulie mazao.
Kwa mfano, ugonjwa ambao viini vyake vinaweza kujificha ardhini, unapotandaza nyasi viini vya ugonjwa visisambae kwa urahisi hasa kama ugonjwa huo unaenezwa kwa njia
ya matone ya mvua au upepo mfano magonjwa ya ukungu (blights) uozo mweusi (Black rots) na mengineyo.

8. Uzuiaji wa magonjwa na wadudu

Kinga ni bora kuliko tiba, inashauriwa kuzuia visumbufu kabla ya kuleta madhara.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Suleiman Mpingama kwa simu
+255765428877.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here