PARACHICHI kama zao la biashara - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 10 November 2016

PARACHICHI kama zao la biasharaMaparachichi yana matumizi mengi yenye faida kubwa kwa wakulima na wadau wengine.
Matunda ni chakula chenye viini lishe bora kama Vitamini (A,B2, C, D,E,K ) na madini ( P,
K, Mn, S ) ambavyo vinalinda mwili, mafuta kwa wingi ( 5-30%) ambayo huleta joto
mwilini, protini (1-5%) ambayo hujenga mwili na kiasi cha calories 250 ambayo huleta
nguvu mwilini. ofauti na matunda mengine, maparachichi ni malighafi ya viwandani
kutengenezea madawa ya ngozi pamoja na vipodozi mfano mafuta ya nywele na ngozi,
shampoo, sabuni na kadhalika
 
AINA ZA MAPARACHICHI

Aina bora za mapararchici ambazo zimefanyiwa utafiti
na kukubalika kwa wakulima na walaji ni pamoja na; HASS, FUERTE, WEISAL,SIMMONDS, EX- TENGERU, IKULU, MWAIKOKESYA, NABALI.
Aina hizi hutofautiana kwenye urefu wa mti, uzaaji wa matunda, ukubwa wa matunda, ladha na muda wa kukomaa. Aina hizi zinazaa matunda mengi na bora pia huchukua muda mfupi kukomaa.Kiasi cha matunda kwa mti kwa msimu ni kati ya 300 hadi 800 kutegemeana na matunzo

Njia bora ya kuzalisha miche ya maparachichi kwa njia ya vikonyo
Njia ya miche bora ni kutumia vikonyo. Faida zinazotokana na njia hii ni:

1/Miti kuchukua muda mfupi kukomaa na kuzaa matunda (miaka 3-3 ½)

2/Miti huwa na umbo na urefu wa wastani

3/Kuzalisha miche yenye tabia moja. Mti haubadili tabia

4/Kuepuka magonjwa hasa virusi

5/Miche mingi kuzalishwa kwa wakati mmoja Kumwezesha mkulima kufanya uchaguzi

Njia za kuotesha miche;

1.Andaa kitalu sehemu wazi na tengeneza kichanja ili kuzuia jua na mvua.
2.Changanya udongo na jaza kwenye viriba
3.Panda mbegu kwenye viriba
4.Panga viriba kwenye kitalu
5.Mwagilia maji
6.Baada ya wiki 2-3mbegu zitaanza kuota
7.Tunza miche hadi kufikia umri wa kubebeshwa miezi 3-4 au unene wa pensile

Ukuaji wa miche hutegemea hali ya hewa. Sehemu za joto mbegu huchipua upesi na miche kukua haraka

Uchimbaji wa mashimo na upandaji wa miche

-Pima nafasi za kupanda ambazo ni: 6m x 5m, 6m x 6m au 6m x 8m. Kwa nafasi hizi unaweza kuyarisha mashimo kati 220-400 kwa hekta

-Chimba mashimo kwa nafasi zilizopendekezwa. Urefu wa shimo sm 75 upana, sm 75 na kina sm 75

- Changanya udongo wa juu na samadi iliyooza kabisa debe moja

-Weka kijiti katikati ya shimo

Acha shimo kwa muda wa wiki 2 hadi mwezi 1 kabla ya kupanda
 
kupanda
Panda miche wakati wa masika
Chagua miche yenye afya nzuri
Ondoa kiribu ( tumia kisu au wembe)
Panda mche kwenye kishimo
Sehemu iliyounganishwa isiguse udongo
Shindilia vizuri na mwagilia maji ya kutosha
 
Mavuno
Kama kila mti utazaa matunda 100 kwa kiwango cha chini, kwa hiyo miti 400 itazaa matunda 400 * 100= 40,000. Ikiwa kila tunda litauzwa kwa shilingi 200 bei ya jumla, fedha itakayopatikana ni sh 80,000 *200 = 8,000,000/= zingatia kwamba hilo zao utavuna kwa muda mrefu sana.
Unaweza kununua miti ya Maparachichi iliyofanyiwa budding tayari na kupanda shambani kwako. Katika muda wa miaka mitatu utaanza kuvuna matunda.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here