Nini tofauti kati ya Dalali na Mchuuzi (broker and dealer) - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 20 November 2016

Nini tofauti kati ya Dalali na Mchuuzi (broker and dealer)

Tukianza na Maana ya Dalali wa soko la hisa la Dar es salaam wanapatikana wapi baada ya kujua ni akina nani katika toleo lililopita

Madalali wa soko la hisa wanapatikana wapi?

Madalali wa soko la hisa kwa sasa idadi yao ni 6 na wote wapo Dar es Salaam. Lakini, kutokana na kukua kwa teknologia na utumiaji wa mawakala, wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali za nchi wanaweza kupata huduma ya madalali bila kulazimika kuja Dar es Salaam.


Ni kweli wawekezaji walio nje ya Dar es Salaam wanawekeza kwa gharama kubwa zaidi ukilinganisha na wenzao walio Dar es Salaam kutokana na muda, gharama za posta, gharama za kutuma au kutumiwa fedha n.k. Juhudi zinafanyika ili kuweza kuwafikishia Watanzania huduma hii kulingana na upatikanaji wa biashara na kukua kwa teknolojia kwa sababu kampuni za udalali zinaendeshwa kwa misingi ya kibiashara.

Kwa nini tunahitaji madalali ili kununua au kuuza hisa?

Kila soko lina taratibu zake, masoko ya mitaji yanahusisha fedha nyingi hivyo ni vyema kuweka taratibu zinazohakikisha uwazi na haki. Madalali hawa ni wataalam katika masoko haya. Wanasaidia kuuza na kununua hisa pamoja na kutoa elimu kwa wawekezaji. Kwa ufupi kuwepo kwa madalali kunawezesha kuwepo na utaratibu na mpangilio mzuri wa mnada na kunapunguza uwezekano wa vitendo vya udanganyifu ambavyo vingeweza kufanywa na wajanja wachache kama kila mtu angeruhusiwa kwenda moja kwa moja kwenye soko la hisa.

Kwa nini tulipe ada ya udalali?

Madalali wanatoa huduma kwa wateja wao kwa kuwasaidia kununua na kuuza hisa zao. Na zaidi ya hapo wanatoa ushauri wa ununuzi na uuzaji wa hisa na mambo mengine yahusuyo soko la hisa. Kutokana na huduma hiyo madalali wanaruhusiwa kwa mujibu wa sheria kutoza ada (Brokerage commission) ambayo ikichanganywa na ada ya Soko la Hisa (DSE) na Mamlaka (CMSA) haitakiwi kuzidi 2% ya thamani ya mauzo au manunuzi husika. 


Nini tofauti kati ya Dalali na Mchuuzi (broker and dealer)?

Mchuuzi (dealer) anaruhusiwa kununua hisa au dhamana nyinginezo kwa niaba yake mweneyewe (principal) na vile vile kwa ajili ya wateja. Dalali (broker) kwa upande mwingine haruhusiwi kununua hisa/dhamana kwa ajili yake. Yeye anafanya kazi kama wakala (agent) kwa niaba ya wanunuzi na wauzaji tu. Dalali anatakiwa kuwa na mtaji usiopungua milioni 10 na 30% kati ya hizo ikiwa ni fedha taslim au aina ya uwekezaji ambao unaweza kugeuzwa kuwa fedha kwa haraka. Mchuuzi anatakiwa kuwa na mtaji isiopungua milioni 20, 30% unatakiwa kuwa fedha taslim au aina ya uwekezaji ambao unaweza kugeuzwa kuwa fedha taslimu kwa haraka. Madalali na wachuuzi wanapewa leseni na kusimamiwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) .

Nini umuhimu wa kuwa na Soko la Hisa nchini?

  1. Soko la Hisa lina nafasi kubwa katika kukuza uchumi wa nchi kama vile:
  2. Kusaidia makampuni kupata mitaji
  3. Kusaidia wananchi kuwa na utaratibu wa kujiwekea akiba Kuongeza maeneo ambayo wawekezaji wanaweza kuwekeza
  4. Ni kipimo cha hali ya uchumi wa nchi
  5. Kusaidia kuongeza utawala bora na uwazi kwenye kampuni zilizoorodheshwa.
  6. Kusaidia kubinafsisha mashirika ya umma.
  7. Kusaidia utambuzi wa bei halisi ya hisa
  8. Huwezesha umilikishaji wa hisa za kampuni kwa umma
  9. Kuwezesha uuzaji kwa urahisi wa hisa

Kwa nini linaitwa soko la hisa la Dar es salaam na sio soko la hisa la Tanzania?

Ni jina tu limechaguliwa kuonyesha kuwa soko hilo liko kwenye jiji la Dar es Salaam. Ingewezekana likaitwa soko la hisa la Tanzania bila kuathiri kitu chochote. Mfano soko la hisa lililoko Kampala Uganda linaitwa Soko la Hisa la Uganda na sio Soko la Hisa la Kampala.

Je, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana inashauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pia?

Ndiyo, Mamlaka inashauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kuna tofauti gani kati ya Hisa na Kipande?

Hisa ni sehemu ya umiliki katika kampuni. Na kipande ni sehemu ya umiliki katika mfuko wa uwekezaji wa pamoja kwa maana ya Amana ya Kikundi (Unit Trust Scheme). Hisa ni sehemu ya umiliki wa kampuni Fulani wakati kipande kinajumuisha mseto wa uwekezaji katika vitega uchumi mbali mbali.

Kuna tofauti gani kati ya kampuni na Mfuko wa Umoja?

Mpango wa uwekezaji wa pamoja kwa muundo wa kampuni ni mpango uliofungwa ambapo hauna fursa kwa mpango kununua vipande kutoka kwa wawekezaji mara baada ya toleo la awali kukamilika. Mpango huu una idadi maalumu ya hisa na vipande kwenye mpango.

Hisa na vipande vya mipango hii huuzwa kwenye masoko ya pili ya mitaji (huorodheshwa soko la hisa). Kama mpango haujaorodheshwa vipande vyake vianuzwa na kununuliwa kwenye soko lisilo rasmi (OTC). Mfano wa mpango uliofungwa ni kampuni ya NICOL.

Mpango wa uwekezaji wa pamoja kwa mfumo ulio wazi au amana ya kikundi ni mpango ulio wazi ambao unawezesha mipango hiyo kununua hisa au vipande wakati wowote mwekezaji akihitaji kuuza vipande. Mpango huu sio kampuni kwani huundwa kwa njia ya Hati ya Amana (Trust Deed) kati ya wadhamini wa mpango na mameneja wa mpango huo. Mfano wa mpango huu ni Mfuko wa Umoja.

Mpango wa uwekezaji wa pamoja kwa mfumo ulio wazi au amana ya kikundi una tofauti kubwa na mfuko wa uwekezaji uliofungwa ama muundo wa kampuni. Tofauti ya kwanza ipo kwenye sheria. Kampuni inaundwa kwa kufuata sheria ya kampuni wakati mfuko wa Amana ya Kikundi unaundwa kwa sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana. Kampuni ikishauza hisa zake haiwezi tena kuzinunua, wenye hisa wanaweza kupata pesa zao kwa kuuza hisa zao kwa watu wengine kupitia soko la hisa kama hisa zimeorodheshwa.

Lakini Mfuko wa Umoja, kama mpango wa wazi unaweza kununua vipande kutoka kwa wawekezaji wake. Tofauti nyingine ni kwenye uwekezaji, kwa mpango ulio wazi uwekezaji hufanywa katika rasilimali za fedha kama hisa, hatifungani na amana za benki tofauti na mpango uliofungwa ambao unawekeza pia katika uzalishaji wa bidhaa na huduma.


Kama ulimisi maana ya Hisa bofya hapa

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here