Nini maana ya Maisha - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 2 November 2016

Nini maana ya Maisha

Maana ya maisha ni mojawapo kati ya masuala kuhusu thamani, madhumuni na umuhimu wa binadamu kuwepo duniani na wa maisha kwa jumla. Suala hilo linaweza kujitokeza katika maswali mengi tofauti yanayohusiana, kama vile Mbona tumekuwepo?, Maisha yanahusu nini? na Ni nini maana ya haya yote?

Binadamu anajiuliza maswali kama hayo hasa anapokabiliana na kifo, kwa mfano msiba wa ndugu au rafiki.

Limekuwa suala kuu la udadisi kwa sayansi, falsafa na teolojia tangu zamani. Kumekuwa na idadi kubwa ya majibu kwa maswali hayo kutoka asili mbalimbali kiitikadi na kiutamaduni.

Maana ya maisha imechanganyikana kwa undani na dhana za falsafa na imani za dini na hugusia masuala mengine mengi, kama vile ontolojia, tunu, kusudi, maadili, hiari, uwepo wa Mungu, roho, na kinachoendelea baada ya maisha haya.

Michango ya sayansi kawaida ni ya moja kwa moja na inaeleza uhalisia kutokana na mambo yanayopimika kuhusu ulimwengu; sayansi inatoa muktadha na mipaka kwa mazungumzo kuhusu mada zinazohusika.

Mbadala ni mtazamo wa kifalsafa unaokabili swali: "Ni nini maana ya maisha 'yangu'?" Thamani ya swali linalohusu kusudi la maisha huweza kuwiana na kuupata ukweli wa mwisho, au hisia za umoja, au hisia ya utakatifu.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here