Ninapataje gawio langu la Faida katika soko la Hisa - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 20 November 2016

Ninapataje gawio langu la Faida katika soko la Hisa


Huu ni muendelezo wa toleo lililopita kuanzia maana ya hisa,gawio na hatifungani, kama ulikosa hayo matoleo bonyeza hapa

Je ninapataje gawio langu?

Gawio ni faida ambayo analipwa mwanahisa iwapo kampuni imepata faida na kuamua tulipa sehemu ya faida kama gawiwo. Njia itumikayo kulipa inategemea na kampuni. Kampuni nyingi zinatumia Shirika la Posta pamoja na mabenki. Ni juu ya mwekezaji kuwasiliana na kampuni aliyowekeza na kutoa habari muhimu kama vile anwani ya posta pamoja na akaunti ya benki.

Kama malipo yatalipwa kwa kupitia njia ya posta basi utapata Hawala ya Posta kupitia anwani yako, na kama malipo yanafanyika kupitia kwenye akaunti ya benki basi utapata hundi au pesa zitaingizwa kwenye akaunti yako. Ni muhimu kutoa taarifa iwapo anwani au akaunti yako itabadilika. Kampuni nyingi zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa zinatoa gawio mara mbili kwa mwaka.

Je ninaweza kuhamisha miliki ya hisa zangu kwa mke au mume wangu?

Ndiyo, hisa zinahamishika. Hisa zilizoorodheshwa Soko la Hisa la Dar-es-Salaam zimehifadhiwa katika Hifadhi ya Dhamana, hivyo uhamishaji wa umiliki ni rahisi kuliko uhamishaji wa kutumia makaratasi na hati. Kwa kanuni za Soko la Hisa la Dar es Salaam, uhamishaji binafsi wa umiliki wa hisa huwezekana wakati dhamana haziko katika mnada. Hivyo uhamishaji wa umiliki wa hisa kutoka kwa mume kwenda kwa mke ni uhamishaji binafsi unaoruhusiwa.


Ninawezaje kununua au kuuza hisa zangu?

Kama unataka kununua hisa ambazo zinauzwa kwa mara ya kwanza (IPO) kuna mawakala maalum ambao huwa wamepewa wajibu wa kuuza hisa kwenye soko la awali. Mwekezaji anatakiwa kujaza fomu ya maombi na kukabidhi pesa kwa wakala kulingana na idadi ya hisa anazotaka kununua na atapewa stakabadhi pamoja na kikonyo cha fomu yako kama uthibitisho.

Kama mwekezaji anataka kunuua hisa kutoka katika soko la pili (DSE), basi itabidi awaone madalali wa soko la hisa. Atawaeleza mahitaji yake. Dalali atatoa ushauri lakini uamuzi ni wake.
Ufuatao ni utaratibu wa kuuza na kununua hisa kaitka soko la pili (DSE):-


Ununuzi


Mwekezaji anayetaka kununua hisa atafuata taratibu zifuatazo:
a) Wasiliana na dalali wa soko la hisa na kumweleza kusudio lako la kununua hisa​
b) Jaza fomu maalum za kununua hisa na kulipia hisa unazotaka kununua​
c) Dalali ataweka fedha kwenye akaunti maalum ya benki kwa ajili ya kununua na kuuza hisa za wateja​
d) Dalali ataweka oda yako ya kununua hisa kwenye mfumo wa kompyuta wa soko la hisa akitumia namba maalum ya mteja.​
e) Iwapo bei unayotaka kununulia hisa itafanana na bei ya mwekezaji mwingine anayetaka kuuza, basi atakuwa amekununulia hisa hizo. Mwekezaji atapokea cheti cha kuthibitisha kuwa ni mwekezaji kwenye kampuni hiyo.

Uuzaji

Mwekezaji anayetaka kuuza hisa atafuata taratibu zifuatazo:
a) Wasiliana na dalali wa soko la hisa na kumweleza kusudio lako la kuuza hisa​
b) Kabidhi hati yako ya umiliki wa hisa kwa dalali​
c) Dalali atahakiki umiliki wa hisa hizo kabla ya kuuza. Kama hisa haziko kwenye hifadhi ya hisa, dalali ataziweka kwenye hifadhi kabla ya kuuza​
d) Dalali ataweka oda yako ya kuuza hisa kwenye mfumo wa kompyuta wa soko la hisa akitumia namba maalum ya mteja. Iwapo bei unayotaka kuuzia hisa itafanana na bei ya mwekezaji mwingine anayetaka kununua, basi atakuwa amekuuzia hisa hizo na mwekezaji atalipwa.

Kuna gharama za kushiriki kwenye soko la pili la hisa. Ushuru unaotozwa ni 2% kwa hisa zinazouzwa kwenye soko la hisa la DSM. Vilevile kuna gharama ya kushiriki kwenye soko la pili la vipande vya Mfuko wa Umoja ambavyo vinauzwa kupitia benki ya CRDB na Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT). Wanunuzi na wauzaji kwenye masoko ya pili hulipa ushuru huu. Kwa upande wa vipande, mwekezaji anatakiwa kulipa 1%. Vipande vya Umoja havijaorodheshwa kwenye soko la hisa la DSM kwa sasa. Mauzo na manunuzi kwa upande wa makampuni ambayo hayajaorodheshwa yana taratibu tofauti za mauzo ya hisa zao.

Nikiwa nje ya Tanzania nitanunuaje hisa?

Watanzania wanaoishi nje ya nchi wana fursa ya kuwekeza kwenye masoko ya mitaji hapa nchini kwenye masoko ya awali na pia kwenye masoko ya pili. Wanaweza kushiriki kwa kumchagua dalali wake ambaye atakuwa anamsaidia kuwekeza. Mwekezaji anatakiwa kuwa na mkataba na dalali wa kumsaidia kuwekeza akiwa nje ya nchi. Mkataba huo utabainisha jinsi ya kupokea fedha na namna ya kuidhinisha manunuzi au uuzaji wa hisa

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here