Mambo muhimu ya kuzingatia katika kulea vifaranga - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 7 November 2016

Mambo muhimu ya kuzingatia katika kulea vifarangaNimuhimu mfugaji kufahamu kuwa kifaranga wa leo ndiye kuku wa kesho  atakaesababisha mafanikio yake na kufanya maisha yasonge mbele bila kikwazo.
Ayubu NnkoUfugaji wa kuku ni moja ya shughuli ambayo imejipatia umaarufu kwa kiasi  kikubwa sana miongoni mwa waku-lima na hata wanaofanya shughuli nyinginezo tofauti na ufugaji peke yake. Ili kuwa na mafanikio ya uhakika ni muhimu kwa mfugaji kuzingatia taratibu zote za ufugaji wa kuku akianzia kwenye utunzaji wa vifaranga ambao ndio kuku wa baadae.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ambayo mfugaji anapaswa kufuata na kuzingatia:


Chakula

: Hakikisha vifaranga wana-pewa chakula sahihi na kiasi kile kina-chopendekezwa kwa umri na uzito hai Husika

Mfano

: Wape chick mashvifaranga wa siku moja hadi wanapofikia umri wa mmoja baada ya hapo watapewa chakula kinachoitwa grower’s marsh/finisher’s mash. Usikae zaidi ya masaa mawili (2) bila ya kuwapa chakula kingine.Usafi

Vyombo vya chakula na maji.

• Hakikisha chakula safi na maji safi vinapatikana wakati wote. Madini, vitamini na viuatilifu vinawekwa kadri inavyoshauriwa na wataalamu wa mifugo.
• Fanya usafi wa kutosha na kuweka dawa kabla ya kuhamishia kuku
• Mazingira ya ndani na nje ya banda ni lazima yawe safi na makavu daima kwani uchafu na unyevun-yevu ni chanzo cha vijidudu vya magonjwa kama vile minyoo na kuhara damu.
• Epuka usumbufu (stress) mahali wanapoishi vifaranga.

Mfano:

a) Epuka Kuondoa mfuniko (hoover) wa brooderkila mara.
b) Epuka pia Kubamiza milango kwa nguvu.
c) Usiruhusu wageni kuingia kwenye banda bila mpangilio.
d) Epuka kukaa muda mrefu bila kuwapa chakula.
e) Kuwepo kwa joto jingi katika chanzo.
f) Utaratibu usiwe wa kubadilika badilika mara kwa mara mfano chakula na maji.
g) Chunguza vifaranga kabla ya kwenda kulala na baada ya kuamka. 
Utaratibu unaokubalika ni kukesha kwa zamu ili vifaranga wasije waka-laliana na hivyo kusababisha vifo vyao. Kazi ya kulea vifaranga ni ya kujitolea sana katika wiki tano za mwanzo.

• Mabandayawe safi na makavu wakati wote ili kuzuia mazalia na chanzo cha maambukizi  kutokana na unyevunyevu.Mwanga na mzunguko wa hewa ya kutosha:
Kuna vyanzo viwili  vya mwanga ambavyo ni
1. Taa ya kandili (kerosene lamp)
2. Taa inayotumia nguvu za umeme (balbu) kama vile (infrared bulbs).

Mwanga na mzunguko wa hewa ndani ya bruda ni muhimu kwani huvutia na kuvishawishi vifaranga kuanza kula.Weka madirisha makubwa yenye kuingiza hewa safi na kutoa ile chafu. Banda lisilo na hewa ya kutosha hucho-chea kuenea kwa magonjwa ya mfumo wa hewa. Andaa nafasi ya kutosha ili kuepuka vifaranga au kuku kurundi-kana.Chakula bora na cha kutosha

a) Wape vifaranga chakula cha kutosha, kizuri na chenye viini lishe vyote.
b) Wape chakula vifaranga kwa vipindi vilivyopangwa badala ya kuwapa mfululizo ili wapate muda wa kutumia chakula walichokula vizuri mwilini.
c) Hakikisha vyombo vya chakula havikai bila chakula. 

Madawa:

• Dawa inatakiwa kuwekwa ndani ya chakula na maji ili kuzuia ugonjwa wa kuharisha damu( coccidiosis).
• Dawa ya kideri ni vizuri ikatolewa wakati vifaranga wamefika na au siku chache baada ya kuingizwa kwenye brooder
.
• Vitamini huandaliwa wakati mwingine pamoja na madawa kama antibiotics ili zichanganywe kwenye chakula chao.
• Zingatia ratiba ya chanjo inayo-pendekezwa na wataalamu.
• Kuku wapewe dawa ya kuzuia maumivu ya usumbufu kwa siku 2-5.

Vifaa ndani ya banda la vifaranga:

Vyombo vya chakula
: Vyombo vya chakula vitawekwa sehemu ifaayo na inayofikika na vifaranga. Hakikisha
vifaa havichafuliwi na kinyesi cha vifa-ranga au takataka zilizomo ndani ya banda. Hakikisha unaongeza vyombo vya chakula na maji kadri vifaranga wanavyozidi kukua na kuongezeka uzito.Vyombo vya maji: Ili kazi ya usafi iwe rahisi umbile na ukubwa wa vyombo vya maji viwe nusu mduara mfano wa mwanzi uliopasuliwa katikati. Mwanzi huu huwekwa katikati ya vijiti viwili vitakavyoushikilia. Vijiti hivi viwekwe katika namna  ambayo ni rahisi kuvirekebisha. Vile-vile kifaa hiki cha maji kinaweza kuwekwa kizibo ambacho kitalegezwa au kuondolewa wakati wa kusafisha. Inashauriwa kuwa vifaa vya kunyweshea viwe na ujazo wa lita tano. Vilevile vifaa hivi viwe vya plastiki ili kuepuka kuotesha kutu.

Ndoana

Hizi ni fimbo za miti au waya ambazo hutumika wakati wa kukama-tia kuku kwa ajili ya tiba au kuwauza.
Toroli au mikokoteni:
Ikiwa banda limejengwa vizuri, toroli linaweza kusadia kupunguza idadi ya masaa  yatakayotumika wakati wa kulisha au kuweka maji.

Kuchagua kundi la vifaranga wenye afya njema

Chagua vifaranga wenye afya njema ambao hutambuliwa kwa kuwa na manyoya makavu, macho maangavu na walio wachangamfu.Chunguza vifaranga wenye kinyeo kilichochafuka na wazubavu na kisha uwatibu. Vifaranga dhaifu, wenye vilema na wagonjwa waondolewe
katika kundi la kuku (culling).Vifaranga wa mayai wahamishiwe kwenye banda la kukuzia wakiwa na umri wa wiki 6-8 ambako watakaa hadi wiki ya 16-18 kabla ya kuhamishiwa  banda la kutagia.

Mabadiliko ya hali ya hewa:

Wakati wa majira ya joto kuku hupunguza kula, hivyo wakati huu inashauriwa kumwaga maji juu ya paa la banda ili kupunguza joto.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here