Kilimo cha Tikiti maji - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 21 November 2016

Kilimo cha Tikiti majiUTANGULIZI
Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama kama matango,maboga na maskwash. Zao la tikiti maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi.Katika shamba la ukubwa wa shamba la ekali moja(1.acre) lililoandaliwa vizuri, kupandwa na kuhudumiwa vizuri mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi
cha TANI 15-36
, ambacho kitamsaidia kupata fedha zitakazo msaidia katika mahitaji  yake mbalimbali na kuondokana na Umasikini.

FAIDA ZA TIKITIKI MAJI
Tikiti maji ni tunda ambalo linapendwa sana na watu wengi duniani. Tunda hili limekuwa maarufu sana duniani kutokana na umuhimu wake kwa afya na mwili wa binaadamu. Waingereza huliita tunda hili kwa majina mawili ambayo ni watermelon na milkmelon. Huko nchini India pia tunda hili hutumika sana na kuna aina mbili ambazo ni watermelon (Citrullus vulgaris) na milkmelon (Cucumis melo). Hapa kwetu Tanzania tunatumia sana aina moja ya tikitimaji ambayo ni watermelon (Citrullus vulgaris). Tunda hili linafaida lukuki ambapo moja ni chanzo cha protini mafuta, nyuzinyuzi, wanga, madini ya calcium, chuma, phosphorus, vitamin A, B6, C, potassium,magnesium na virutubisho vingine vingi.

ENEO
Chagua eneo ambalo halina historia ya kuwa na magonjwa ama wadudu wanaoshambulia tikiti maji.Eneo ambalo maji yanapatikana kwa urahisi kwaajili ya umwagiliaji wa tikiti maji litafaa,pia eneo lisilo na udongo wenye chumvi chumvi ama maji yenye chumvi chumvi.

KUANDA SHAMBA
Baada ya kuchagua aina ya mbegu unayohitaji kupanda, inashauriwa kulima shamba na kuacha kwa muda wa kipindi kitakachoruhusu nyasi na magugu mengine kuoza kabla ya kupanda.Hii inasaidia majani na magugu kutoota upesi pindi ukipanda miche yako ya matikiti.Hakikasha kuwa shamba lako limelimwa vizuri na udongo kulainika, udongo uwe umechimbuliwa kiasi cha inchi 8-10 kwenda chini.Ukishalima shamba lako vizuri kwa kuvunja vunja udongo na pia andaa matuta yenye upana wa mita 2 na urefu kwenda juu sentimita 30 ili kusaidia mizizi ya tikiti kukua vizuri na kuzuia maji kutwaama hasa katika kipindi cha mvua

MAHITAJI YA MBEGU
Kwa shambari la ekari moja andaa mbegu 4,000 mpaka 6,000
sawa na gram 300 za mbegu
au wastani wa kilo 3 hadi 4
ambapo jumla ya gharama za mbegu ni kati ya tsh 200,000 hadi
tsh 300,000
.
MAHITAJI YA TIKITIMAJI

Tikiti linakua vizuri ktk udongo unaoshika maji vizuri lakini yasio tuama na kuruhusu mzunguko mzuri wa hewa na maji.Udongo wenye pH 5.8-6.6.Tikiti halistawi vyema ktk baridi na linahitaji joto la udongo kiasi cha 180c-290c.Joto chini ya 180c na juu 290c litaathiri kuota kwa mbegu na ukuwaji wa mmea.Katika kipindi cha ukuwaji tikitimaji linahitaji unyenyevu wa udongo wakati wote lakini maji yakizidi ktk udongo wakati wowote wa ukuwaji na uwekaji wa matunda hupelekea  upasukaji wa matunda na kupunguza mavuno na ubora wa matunda

Aina  za matikiti maji


 NEGRA F1
Aina hii ya matikiti maji ni ya  mviringo yenye mazao na sifa nzuri”
Ubora wake
 • Yana mazao mazuri, na uwezo wa kukupa tani 46 kwa kila ekari
• Ni matamu sana na yenye wekundu wa kung’ara
 • yanakomaa katika muda wa siku 100-120
• Ni mviringo na yenye rangi ya kijani kibichi na hutoa matunda yenye  mizani kati ya kilo 7-10
 • Mmea hukua haraka na una mazao mazuri
 •Yamezungukwa na nyama ngumu, nzuri, yenye kukuwezesha  kusafirisha hadi sehemu za mbali
 • Yana kinga dhidi ya  ugonjwa wa mnyauko unaosababishwa na  vimelea aina ya Fusari (Fusarium wilt)


SENTINEL F1 

  ni aina mpya ya matikiti ya mviringo marefu” 
Ubora wake
• yanaweza kuzaa sana hadi tani 50 kwa kila ekari
• Ni marefu, yameshiba na yana rangi ya pundamilia
 • ni tamu, yan wekundu uliokolea na nyama iliyo na maji mengi
 • Yanawezakutoa matunda ya kufanana na yaliyo na uzani kati kilo 11 - 14
• Matunda yana nyama nyingi na umbo inayokuwezesha kusafirisha masafa marefu
 • yana kinga dhidi ya maradhi ya vimelea aina ya Fusari (Fusarium wilt Race 1)
 • yanakua tayari katika muda wa siku 100 -120 

Mbali na kuwa na faida mbali mbali kiafya tikiti maji linaweza kumtoa mkulima wa kawaida katika umaskini. Hii kutokana na sababu zifuatazo.


·   Tikitimaji ni zao la bustani linalochukua miezi 3-4 kuvunwa, hivyo kwa mwaka linaweza kuvunwa mara 3 hadi 4
·         kwa ekari moja mavuno ya tikiti maji ni matunda 2000 - 8000  au zaidi kwa miezi 3-4 kutokanana uangalizi wa mkulima katika shamba ikiwa ni kutumia mbolea kama inavyo takiwa, kuzuia wadudu na magonjwa, n.k. Pamoja na nafasi iliyotumika katika upandaji (1x1m, 2x2m, 1.5 x 1.5m).

JINSI YA KUJUA FAIDA
Katika maeneo mengi ya Tanzania bei ya tikiti maji lenye sifa nzuri ni shilingi 2,000/= hadi 3,000/=

kwa bei ya 2,000/= na mavuno ya 2000 matunda/ekari (Matunda mazuri)
Baada ya mavuno utajipatia kiwango cha chini kisichopungua jumla ya Tsh.4,000,000/= kwa mwaka ni 12,000,000/= kwa mavuno ya mara tatu kwa mwaka kwa ekari.

Gharama hii itaenda juu zaidi ama itapungua kutegemea na idadi ya matunda uliyoyapata katika ekari mmoja na bei ya muuzaji. Hivyo unaweza ukapata faida kubwa zaidi ukiongeza uangalizi wa shamba lako na kufuata utaratibu katika ulimaji wa zao hili.

MAHITAJI
Tikiti maji linahitaji mbolea, maji, kemikali za kuua wadudu na magonjwa pamoja na maandalizi mabali mbali ya shamba ambavyo gharama yake haizidi Tsh. 500,000/= katika uangalizi mkubwa

FAIDA
Hivyo mkulima katika uangalizi wa mzuri ana uhakika wa kupata faida ya Tsh. 3,500,000/=  na zaidi kila baada ya miezi 3-4.  No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here