Kilimo cha Pilipili Hoho na Manga - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 2 November 2016

Kilimo cha Pilipili Hoho na Manga

Utangulizi
Pilipili ni kiungo kikali, hutumiwa kwa kukoleza mchuzi na vyakula mbali mbali. Pilipili zinaweza kupikwa zikiwa nzima au kukatwakatwa na kutumiwa katika kachumbari; au kuwekwa kwenye siki na achali, au kusagwa na kutumia unga wake.
Hili ni zao la nchi za kitropiki, na hutumiwa sana na wakazi wa Bara Hindi, Mashariki ya Mbali. Amerika ya Kusini na Afrika ya Tropiki. Pilipili huwekwa katika makundi makubwa mawili, yaani:
hoho
Pilipili Hoho (Hot Pepper)- Hizi ni ndogo ndogo, ndefu, nyembamba, na kali sana. Aina zinazojulikana zaidi ni Green Chilli, Cherry Pepper, Long Cayenne na Tabasco.
Pilipili Manga (Sweet Pepper)- Hizi zina umbo kubwa, nyama nying, mviringo na ndefu kidogo, siyo kali. Aina zinazojulikana zaidi ni Sweet, Neapolitan, Keystone, Giant, Ynlo Wonder na california wonder.
Kupanda
Mbegu hupandwa kwenye kitalu ambamo hukaa kwa muda wa majuma manane hadi kumi. Kisha miche hupandikizwa bustani kwa umbali wa sentimeta 45 kwa 90.
Kuvuna
Umri wa kuvuna zao hili hutegemea aina ya pilipili na matumizi yake. Aina ambayo ni kubwa na tamu kwa kawaida huvunwa kabla haijapevuka na kugeuka rangi yake. Pilipili katika hali hii hutumiwa zaidi kwenye michuzi, kachumbali na kutiwa kwenye makopo.
Pilipili kali, ambayo mara nyingi ni ndogo ndogo, kwa kawaida huvunwa baada ya kupevuka na kuwa nyekundu. Halafu hutumiwa katika mapishi na vyakula mbali mbali, lakini sehemu kubwa zaidi hukaushwa na kusagwa ili kupata unga wake.
imageskgy
Magonjwa
Damping- off, Bacteria Spot, Fusarium wilt na Antracnose, ni miongoni mwa magonjwa yashambuliayo zao hili. Tuseme magonjwa ya pilipili ni sawa na ya Nyanya. Hivyo njia za kupigana nayo ni sawa.
Wadudu: Wadudu ambao hushambulia zao hi wengi, lakini walio wabaya zaidi ni Aphids, Cut worm, Flea beetle, Pepper weevil na Pepper Maggot.
Kinga: Parathion 1% au Chlrdane 5%. Dawa itumiwe mara wadudu watokeapo na kurudiwa kila baada ya siku 7.
[23:31, 6/11/2016] +255 653 759 223: KUJENGA MTANDAO WA BIASHARA
Mtandao (network) ni muhimu sana katika kujenga biashara yako na katika kujijenga katika kazi/career yako. Mtandao unakusaidia kupata rasilimali, kupata taarifa za masoko, kupata taarifa mbalimbaili na kukamilisha mambo yako kwa urahisi. Ili kujenga Mtandao tunahitaji kufanya mambo yafuatayo:
1. Jenga mahusiano na watu ambao mnaweza kusaidiana kibiashara au kikazi. Mahusiano yanajengwa kwa kufahamiana na watu sahihi na kuwa na mawasialiano nao.
2. Shiriki katika matukio yatakayokukutanisha na watu-semina, mikutano, michezo, maonyesho, kusali, sherehe za muhimu, chakula cha jioni na vikundi vya msingi. Usijifungie sana.
3. Tengeneza utambulisho wako (business cards) na wa biashara yako (vipeperushi) na wapatie watu wanaoweza kuwa rasilimali kwako.
4. Tumia njia za kimtandao kuwasiliana na wateja wako, marafiki na jamii kwa ujumla (simu, email, instagram, blog, face book n.k). Uwe unajibu ujumbe na kufautilia mahusiano yako kwenye mtandao.
5. Tengeneza mtandao wa marefa wako (referees) ambao watakuwa mabalozi wako.Watu hawa wanatengenezwa kwa kujenga mahusiano ya karibu na hata kuwaomba wakutangazie biashara yako.
6. Uwe na takwimu/database za wateja wako na watu wa karibu. Kila kukiwa na matukio muhimu kama sikuu, kumbukumbu mbalimbali n.k wasalimu na kuwatakia kila la heri.
7. Toa huduma nzuri na jenga tabia ya kufuatilia jinsi huduma yako inapendwa sokoni. Kukiwa na bidhaa mpya au huduma yeyote mpya wajulishe wateja wako. Usikubali ukapita muda mrefu bila kuwa na kitu cha kukuweka karibu na wateja wako.
8. Kila unapopata fursa jitambulishe vizuri wewe pamoja na biashara yako. Kwa wanaotaka zaidi soma kitu kinaitwa “elevator speech” kwenye mtandao (http://www.businessballs.com/business-networking.htm ). Kwa kifupi kama uko sharp dakika 3 za kukutana na mtu kwenye lift zinatakiwa zitoshe kujitambulisha wewe na biashara yako na kupata mawasiliano ya mhusika.
9. Jenga tabia ya kusaidia watu wengine. Kabla ya kupokea jifunze kutoa, utapata mtandao mkubwa sana.
10. Timiza ahadi zako na uwe mwaminifu katika mahusiano yenu na kuhusu taarifa za wenzako.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here