Kilimo cha Kabichi, faida lukuki kiuchumi na kiafya - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 10 November 2016

Kilimo cha Kabichi, faida lukuki kiuchumi na kiafya


Kabichi hulimwa kwa wingi zaidi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tanga, Iringa na Mbeya. Uzalishaji wake ni wastani wa tani 242,771 kwa mwaka.

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUZALISHA

Mazao mengi na bora ya kabichi hupatikana iwapo kanuni za kilimo bora zitazingatiwa wakati wa uzalishaji. Baadhi ya kanuni hizo ni kama zifuatazo:
 

Kuchagua aina ya kupanda

Panda aina bora kufuatana na mahitaji ya soko. Pamoja na mahit
aji ya soko, ni vema kuchagua mbegu zinazovumilia magonjwa, mashambulizi ya wadudu na zinazokomaa mapema.

Kudhibiti magonjwa na wadudu

Kagua shamba ili kuona kama kuna dalili za mashambulizi ya wadudu na magonjwa. Uonapo dalili za mashambulizi chukua  tahadhari mapema kwa kunyunyuzia dawa kabla madhara hayajawa makubwa.

Lengo la kudhibiti magonjwa na wadudu ni kupata mazao mengi na bora yanayoweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu.

Kuweka matandazo
Weka matandazo ili kudhibiti magugu na kuhifadhi unyevu. Matandazo pia hupunguza palizi ya mara kwa mara inayoweza kusababisha mizizi kukatwa na bila kusahau kuweka mbolea kabla ya kupanda .

Kumwagilia maji
 
Kagua udongo ili kuona kama kuna unyevu wa kutosha, ikiwa udongo hauna unyevu wa kutosha,mwagilia maji inavyotakiwa. Kabichi zikikosa maji ya kutosha huchelewa kufunga na huwa na
vichwa vidogo, na zikipata maji mengi ghafla, vichwa hupasuka

upandaji

Katika mstari hadi mstari inatakiwa iwe sentimita 60-75. Kutoka mmea hadi mmea ni sentimita 30-60. Pia sentimita 75-90 inaweza kutumika kati ya mstari na mstari

MAANDALIZI KABLA YA KUVUNA

Kukagua shamba

• Kagua shamba kuona kama kabichi zimekomaa Kabichi hukomaa katika kipindi cha miezi miwili mpaka mitano tangu kupandikiza miche.
Dalili za kabichi zilizokomaa

v  Vichwa hufunga na huwa vigumu
v   Uzito wa kabichi huongezeka. Kabichi iliyokomaa huwa na uzito wa kilo moja na nusu hadi nne kutegemea na aina ya mbegu.

Kuvuna
 
Uvunaji hufanyika kwa kutumia mikono ambapo kisu kikali hutumika.
v  Vuna kwa kukata shina sentimita mbili hadi tatu kutoka kwenye kichwa cha kabichi.
v  Ondoa majani ya nje na acha majani mawili au matatu ya kijani kwa ajili ya kuzuia kabichi zisikwaruzike au kuoza wakati wa kusafirisha.
v  Vuna wakati wa asubuhi au jioni kuepuka upotevu wa maji kwenye kabichi.

MCHANGANUO WA FAIDA

Kiwango cha juu kwa mazao bora utakayovuna ni kabichi 8000 kiwango cha kati kabichi 6000 
Kabichi 6000 kwa bei ya shamba ni tsh 250 ( soko likiwa zuri ) kwa kabichi moja Mara 6000 ni tsh milioni moja na nusu kwa miez 3 tufanye ulimwagilia kwa mashine ambayo mafuta yaligharimu laki moja na shamba 50 elfu na mbegu laki moja na umetumia muda wako wewe mwenzangu ambae huna mtaji wa kutosha ni dhahiri utapata mtaji wa kulima heka 5 awamu inayofata…

VIJANA TUANZE KULIMA KILIMO CHA KISASA TUJIKWAMUE KUTEGEMEA MPAKA TUONGOZE WENYEWE SOKO LA BIASHARA

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here