JINSI YA KUPATA WAZO LA BIASHARA LINALOWEZA KUKUTAJIRISHA. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 2 November 2016

JINSI YA KUPATA WAZO LA BIASHARA LINALOWEZA KUKUTAJIRISHA.

Humu duniani kuna watu wenye akili nyingi sana za kidarasa lakini hawana mawazo yoyote ya kijasiriamali , Unakuta mtu haoni fursa zinazomzunguka wameng’ang’ania tu kwenye ajira wanazozifanya lakini anashindwa kuona fursa nyingi zilizomzunguka.

Lakini pia kuna watu hawajasoma hata kidogo lakini ndio hao wanaibuka na mawazo yanayowatoa, Kuna rafiki yangu mmoja aliniambia kuwa zaidi ya asilimia 70 ya matajiri wote katika nchi ya Tanzania wameishia darasa la saba. siri kubwa ya hawa ni ule uwezo waliojijengea wa kuziona fursa na kuendelea kuzitumia.
Hivyo basi katika darasa hili tukimaliza utakuwa umepata mwanga mkubwa sana wa jinsi ya kutumia fursa zinazokuzunguka. na kama utakuwa na swali nijuze nami nitakujibu kuptia e mail yangu

WhatsApp-Image-20160606 (7)

Inawezekana umeshawahi kupita sehemu siku za nyuma ukaona kuna mbuga au kichaka lakini baada ya miaka miwili au mitatu ukapita tena sehemu ile ukakuta kuna fremu za maduka au supermarket pale,. Tofauti pale ni nini! wakati wewe ulipoona kuna kichaka au mbuga mwenzio aliona kuna fursa ya kibiashara .
Hivyo basi natuamini hili somo la leo litakusaidia wewe kukujengea jicho la kuona fursa, Hivyo basi tutakupatia mbinu ambazo zitakusaidia wewe kuziona fursa,

Hivyo basi tega sikio inawezekana siku ya leo ndio siku ya kukuletea mabadiliko makubwa katika maisha yako.
Njia hizo ni kama zifuatazo

1. ANZA NA FAMILIA YENU
Hapa namaanisha kuwa endapo wazazi wako wanafanya biashara fulani ambayo tayari imekwisha onyesha mafanikio basi huna haja ya kuhangaika na kujaribu kwenda sehemu nyingine au kujaribu kufanya kitu kingine, unaweza ukaichukua ile biashara kama ilivyo na ukaamua wewe kuifanya iwe bora zaidi,
Sisemi uwe na wazo la kuiga lakini nachosema ni kwamba watu wengi wanapokuwa na wazo la biashara kwenye vichwa vyao huwa wanakuwa na theories hilo wazo halijakuwa proven (halijahakikishwa bado) uwezekeno wa kushindwa uko pale pale kwa hiyo leo hapa nataka nieleze kidogo kama mimi nilivyoziona nilipotembea mikoani na kugundua vitu mpaka leo hii nipo chuo na nina biashara tayari nzuri,
Sasa unapokuwa na biashara ya mjomba wako au ndugu yako ambayo umeshaiona tayari imefanikiwa maana yake ni kwamba na wewe unaweza kuifanya na ikawa na mafanikio mazuri.

Kwa mfano, Je unamfahamu mtu tajiri kuliko wote hapa Tanzania ambaye ni Mohamed Dewj, ambaye anaongoza kampuni ya Mohamed interprises ,
Yeye baada ya kumaliza masomo yake nje ya nchi aliporudi hapa nyumbani aliamua kuchukua biashara ya baba yake alichofanya akaipandisha ile kampuni, akaijengea mazingira mazuri, akaipanua na kwa sasa ile kampuni ndio mwajiri mkubwa kuliko makampuni yote hapa Tanzania ina waajiriwa zaidi ya 24000 na ndio kampuni kubwa kuliko yoyote ambayo sio ya kiserikali. na kusababisha Dewj kuingia kwenye orodha ya mabilionea duniani,

Sasa yeye alichofanya ni kuchukua biashara ya baba yake na sio wazo jipya.Nirudie tena kusema, hata mchanganuo wako wa biashara uwe mzuri kama hujaanza ile biashara yako hiyo tunaita nadharia, Kwa hiyo nenda na mawazo ambayo yamehakikishwa, hivyo basi tafuta matunda ambayo yapo chini wewe kuyafikia halafu yafanyie kazi.

Mtu tajiri kuliko wote duniani anapenda kusema ”Take an ordinary idea but give it an extra ordinary execusion ” jipatie wazo la kawaida kabisa lakini lipatie utendaji wa tofauti. ” kwa hiyo unaweza kuchukua wazo la kawaida tu na ukilifanyia kazi vizuri utakuwa na mafanikio..
Lakini vipi kama huna ndugu, shangazi, mjomba mwenye biashara . kuwa nami kwenye hizi mbinu nyingine zinazofuata

2.KUPITIA KUSAFIRI
Siri mojawapo ambayo watu hawajaifahamu leo hii ni kwamba unaweza kupata wazo kwa njia ya kusafiri. Kwa mfano wewe unakaa Arusha na ukaenda Dar es salaam ukaona kuna biashara inafanyika Dar es salaam ambayo haipo Arusha, unaweza kuipeleka biashara ile Arusha na hivyo ukawa wa kwanza kuitambulisha biashara, hivyo hii inaweza ikawa njia nyepes na ya haraka kukutajirisha. Kama uko Mbeya nenda Iringa, kama uko Iringa nenda Mtwara amini usiamini kusafiri ni njia nzuri sana la kukupa wazo zuri la kukutajirisha
Kwa hiyo jiwekee utaratibu wa kusafiri, Hata kwa wewe muajiriwa kila unapopata likizo usiache kusafiri maana katika kusafiri unaweza kupata mawazo mengi ya Biashara.

Nikuulize swali, Je Utaanza lini kusafiri,? Na utakwenda wapi kwa ajili ya kutafuta mawazo? Mara nyingi
 wazo zuri halikufuati ulipo.

3. KUPITIA VITU UNAVYO VIPENDA KUFANYA (hobbies)
Swali la msingi la kuanza nalo ni je wewe una hobi gani/ unapenda kufanya vitu gani? katika vitu hivyo unavyopenda kuvifanya Je tunaweza kugeuza kimojawapo kikawa kinakuletea Fedha?
Kijana aliyeanzisha Clouds Fm Mr Joseph Kusaga yeye alikuwa ni Dj ambaye alikuwa anapiga muziki kwenye maklabu ya zamani kama kilimanjaro Hotel na sehemu zingine na alikuwa akitoka shuleni wakati wa weekend alikuwa akipiga muzikina watu wanafurahi na kucheza. na hakuwahi kujua kama ile kai yake au u Dj ingeweza kumpelekea kuwa mmiliki wa kituo cha redio pamoja na televisheni,

Kwa hiyo jambo la kuangalia hapa usidharau jambo unalolifanya na kuona kama unapoteza muda. Mfano unaweza ukawa na hobi ya kupika vizuri hiyo inakuashiria kuwa unaweza kuwa na restaurant.
Umuhimu mwingine wa kufuata hoby ni kwamba utaifanya ile kazi kwa bidii sababu ni kitu ambacho unakipenda toka moyoni mwako.
Kwa hiyo jambo la msingi jiulize una hobi gani? Fuata ile hobi uliyonayo, Tumia hobi yako kutatua matatizo uliyonayo kibiashara

4.KUPITIA MARAFIKI NA MAZUNGUMZO
Baada ya kuangalia njia hizo 3 tuangalie njia ya 4.
Wakati mwingine kupata wazo unatakiwa Kuwa makini sana kusikiliza watu wanaongelea nini. Unaweza ukapata wazo kwa njia ya kusikiliza / kupitia mazungumzo. na usikurupuke unaposikia wazo kwanza weka mbinu ya kwanza ambao ni kulichimba lile wazo,
Pia kama umetindikiwa kabisa mawazo lakini una marafiki wengi jaribu kuwauliza kuwa wanaona biashara gani ni nzuri? huwez kukosa rafiki hata mmoja au wawili watakaokupa wazo zuri la biashara.
Kwa hiyo kupitia marafiki tengeneza wazo la biashara ambayo yanaweza kukusaidia, tafuta rafiki tajiri ili aweze kukusaidia

5. ANGALIA KERO NA SHIDA ZILIPO KWENYE JAMII YAKO NA UZITATUE
Na mwisho kabisa ni kuangalia kwenye jamii yako kuna tatitzo gani, mfano mtaani kwenu hakuna nini? tumia fursa ile kupata wazo la biashara yako.
Huenda uko sehemu ambako hakuna M-pesa au Tigo pesa. , tumia nafasi hiyo kuweka huduma hizo.
ANGALIA WATU WA ENEO LAKO WANAPENDA VITU GANI ZAIDI
MFANO MAVAZI FULANI CHAKULA FULANI hata cha ASILI YAO MAREMBO FULANI KINYWAJI FULANI na vitu kama hivyo

7; FUNDISHA WATU KITU KIPYA HALAFU WEWE NDO UTAKUA SUPPLY WAO
Mfano wakulima au wafugaji wafundishe ukulima wa zao jipya halafu wewe tsfuta soko lake watakuuzia
Au ufugaji wa kisasa wewe utanunua kwao na kuuza
Na vyengine kama hivyo

NOTE
Ili mwanadamu aweze kufanikiwa anahitaji vitu vitatu.
1. Watu
2.Fedha
3. Wazo

Bahati vitu vyote vitatu huwa haviji kwa wakati mmoja, kuna wakati mwanadamu atakuwa na fedha hana watu na hana wazo, au ana wazo na hana fedha wala watu. Cha muhimu sana katika vitu vyote n kimoja nacho ni wazo sio wazo tu ila ni wazo la biashara. watu wengi duniani wamehangaika huku na kule kufikiria wazo la biashara ni nin.

Wazo la biashara ni tatizo ambalo likitatuliwa watu watakupatia fedha au malipo fulani, Afrika ni bara lenye matatizo mengi sana kuliko ulaya na marekani, kwa hiyo kuwepo kwa matatizo mengi sana Afrika ina maana Afrika kuna mawazo mengi sana ya biashara kama tu watu watajaribu kuyatafutia matatizo hayo suluhisho,
Kwa hiyo unapotembea , unaposikiliza watu sikiliza wanalalamika kitu gani, sikiliza kilio chao kikubwa ni nini? malalamiko ya watu ni biashara, matatizo ya watu ni biashara, palipo na matatizo mengi kuna mawazo mengi ya biashara.

Kwa hyo kitu kikubwa ni kusikiliza watu wanalalamika nini na unaposikia watu wanalalamika usiwe sehemu ya walalamikaji bali uwe sehemu ya kutafuta jinsi ya kuondoa tatizo hilo, na utapofanikiwa kuliondoa tatizo hilo wanadamu hawana jinsi nyingine isipokuwa ni kukulipa, na watakapokuwa wakikulipa na wewe unatoa suluhisho la tatizo tayari biashara imekwisha kuzaliwa,
Hivyo basi nakusihi popote ulipo zunguka kila mahali uangalie watu wana matatizo gani na wewe utafute suluhisho la tatizo hilo, ukilifanya jambo hilo peke yake utakuwa umekwisha kufanikiwa.
By Shafii Said

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here