jinsi mawazo yetu na hatimaye tabia zetu zinavyoathiri hali zetu za kifedha. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 3 November 2016

jinsi mawazo yetu na hatimaye tabia zetu zinavyoathiri hali zetu za kifedha.


1.Fedha ni wazo.
Watu wengi wamekuwa wakifikiri fedha ni yale makaratasi ambayo wanabadilishana nayo na wengine. Fedha siyo karatasi jekundu lililoandikwa shilingi elfu kumi. Bali fedha ni wazo ambalo lina thamani ya kilichoandikwa kwenye karatasi. Kwa mfano kama mimi nina bidhaa ninayouza ambayo gharama yake ni shilingi elfu kumi, maana yake kuna wazo ambalo nimeweza kuligeuza bidhaa na thamani ya wazo hilo ni elfu kumi.
Kwa kujua hivi utaweza kuchukua hatua sahihi, kwa mfano kama kwa sasa una changamoto ya kifedha, maana yake huna mawazo yenye thamani kubwa kifedha. Anza kuja na mawazo hayo na utatatua changamoto yako kifedha.

2. Fedha siyo lengo.
Hakuna mtu aliyepata utajiri mkubwa kwa kuweka lengo kuu kuwa kupata utajiri. Hapa ndipo watu wengi wanapokosea na kukuta wanahangaika maisha yao yote wasipate utajiri wanaotaka. Utajiri siyo lengo, bali utajiri ni matokeo ya wewe kukamilisha malengo yako mengine kwenye maisha. Lengo lako kuu lisiwe kupata utajiri, bali kutoa thamani kwa wengine.

3. Hali yako ya kifedha ni matokeo ya wewe mwenyewe.
Hali ya kifedha uliyonayo sasa ni matokeo ya maisha yako kwa ujumla. Upo hapo ulipo kifedha kutokana na mawazo, mtazamo na matendo uliyonayo kwenye maisha yako linapokuja swala la fedha. Maamuzi unayofanya kila siku kwenye maisha yako, yanaathiri eneo lako la kifedha. Mtazamo wako juu ya kazi, utajiri na maisha kwa ujumla, unachangia hali uliyonayo.

4.     Fedha haiwezi kununua furaha.
Hii ndiyo kauli ya kijinga kabisa ambayo masikini wamekuwa wanajifariji nayo, kwamba fedha haiwezi kununua furaha. Ni kweli fedha haiwezi kununua furaha, kwani nani alituahidi fedha inanunua furaha. Furaha ni matokeo ya mtu kuwa na maisha bora, ambapo fedha pia inachangia kwenye ubora wa maisha. Hivyo acha mara moja kujifariji kwamba ni vizuri huna fedha kwa sababu hainunui furaha, wewe ishi maisha yako vyema, fanya kazi zako kwa ubora na fedha na furaha vitakuwa matokeo ya maisha yako.

5. Thamani ya fedha ipo kwenye mzunguko.
Fedha ni kama maji, matone machache unaweza kuyadharau, lakini matone haya yanapoendelea nayaweza kuzaa mfereji, mifereji inapeleka mto a mtu kwenye ziwa au bahari. Fedha inafuata mtiririko huo, mtu anaweza kuanza na kiasi kidogo mno, kwa kukizungusha sawasawa, kwenye biashara au uwekezaji baada ya muda kiasi kile kinakua sana. Wale wanaozungusha fedha ndiyo wanaopata thamani yake. Wale wanaopata na kutumia pekee, wanabaki kuwa masikini. Usikubali fedha yoyote inayopita kwenye mikono yako iondoke yote, ondoa hata tone moja na zungusha.

6. Utajiri unaanzia kwenye akili, siyo mfukoni.
Watu wengi hufikiri kwamba wakishapata fedha basi watakuwa na akili ya fedha. Lakini hiko ni kinyume, unakuwa na akili ya fedha ndiyo unaweza kuzishika kwa nidhamu na kufikia utajiri. Matajiri wote wana mtizamo tofauti kabisa katika swala la fedha ukiwalinganisha na masikini. Matajiri wanaijua misingi ya fedha na hawaikiuki, ila masikini, hawataki hata kujua misingi hiyo, wanaendesha maisha kama yanavyowajia.
Kitu cha kwanza kinachowatofautisha masikini na matajiri ni mtazamo wa kifedha. Na mtazamo huu unaanzia kwenye imani. Imani ya fedha ndiyo imekuwa kichocheo cha watu kufanikiwa na kikwazo kwa wengine kufanikiwa.

7. Ufahamu wa kifedha ni muhimu.
Kikwazo kingine kwa watu kupata fedha ni ufahamu walionao kifedha. Watu wengi wana ufahamu mdogo sana kuhusu fedha, na ufahamu huu ni kile kiwango ambacho wamezoea kupata. Kwa mfano mfanyakazi anayelipwa milioni moja kwa mwezi, ameweka ufahamu wake wa kifedha kwenye kiwango hicho, hivyo hajawahi kufikiria vipi kama angeweza kupata mara kumi ya kipato alichonacho sasa. Hivyo pia kwa wafanyabiashara, wengi wanapata kipato kile kile kwa sababu ndiyo ufahamu wa kifedha walionao.
Ili kukuza ufahamu wa wako wa kifedha, anza kufikiria kama kipato chako kingekuwa mara kumi ya unachopata sasa. Fikiria ni kwa namna gani unaweza kuongeza kipato chako kwa kiasi hicho, utaanza kuzioana fursa zaidi za kuongeza kipato chako.

8. Sikiliza wengine lakini chukua maamuzi yako.
Linapokuja swala la fedha, kila mtu ana ushauri wa kutoa. Hata watu ambao hawajawahi kutengeneza fedha kwenye maisha yao, wanaweza kuwashauri wenzao namna ya kutengeneza fedha. Hivyo watu wengi watakushauri mengi kuhusu fedha, lakini fanya maamuzi ambayo unajua ni bora kwako na utaweza kuyasimamia.

9. Utajiri ni mchakato, siyo ajali au kitu cha haraka.
Hakuna kitu kinawapoteza masikini kama kushindwa kuelewa hili. Watu wamekuwa wakifiria kwamba kuna njia ya haraka ya utajiri ambayo matajiri wanaijua ila wao hawaijui. Utawasikia wanaongea mambo ya kijinga kama freemason na bahati. Lakini wale waliopaya utajiri, wanajua ni kwa namna gani imewachukua muda kupata utajiri huo.
Katika kutafuta njia hizo za mkato, masikini wengi wamekuwa wakiishia kutapeliwa hata ile fedha kidogo waliyonayo. Jua kwamba unahitaji muda ili kufikia uhuru wa kifedha, na usitafute njia ya haraka au njia ya mkato.

10.  Fedha haimbadilishi mtu, bali inamwonesha jinsi alivyo.
Imekuwa ni kawaida kusikia watu wakisema mtu fulani tangu amekuwa na fedha amebadilika sana. Labda amekuwa na roho mbaya kuliko hapo awali. Hivyo kuna ambao wamekuwa wanatumia hii kama sababu ya wao kutokupata fedha, wakiogopa zitawaharibu na kuwagombanisha na wengine.
Ukweli ni huu, fedha haina tabia yoyote, tabia wanazo watu, fedha inachofanya ni kuzionesha zile tabia za watu, jinsi zilivyo bila ya kificho. Kadiri mtu anavyokuwa na fedha ndivyo anavyokuwa na majukumu mengi, na kuweza kuwaathiri wengi. Hivyo kama alikwa na tabia mbaya basi itawaathiri wengi.

11.  Njia pekee ya kupata fedha ni hii; TOA THAMANI.
Fanya ufanyavyo, lakini mwisho wa siku kanuni ya fedha ni hii, unalipwa kulingana na thamani unayotoa. Nukta. Hakuna namna yoyote unavyoweza kwenda kinyume na kanuni hiyo. Unalipwa unacholipwa sasa kwa sababu hiyo ndiyo thamani unayotoa. Kama unataka kuongeza kipato chako, ongeza thamani unayotoa kupitia kazi yako au biashara yako.
Hapa napo kuna matatizo yanayowatofautisha matajiri na masikini, masikini anasema nikianza kulipwa vizuri ndiyo nitatoa thamani kubwa, tajiri anasema nitaanza kutoa thamani kubwa na najua nitalipwa vizuri. Sasa niambie wewe mwenyewe, kama ungekuwa umeajiri watu hao wawili, ungemwongezea yupi kipato?

12. Fikra hasi zimetawala sana jamii zetu, hasa linapokuja swala la fedha.
Kuna baadhi ya maeneo ukianza kuongea kuhusu fedha unaonekana kama mtu mwenye tamaa. Pengine unakatishwa tamaa kwamba unachofikiria hakiwezekani. Unahitaji kuwa makini sana na jamii inayokuzunguka, kama ni watu ambao wana fikra hasi kuhusu fedha, watakurudisha nyuma. Linda sana fikra zako dhidi ya fikra hasi zinazosambaa kwenye jamii.

13. Fanya kile unachopenda kufanya, ndipo utajiri wako ulipo.
Tatizo kubwa kwenye jamii zetu ni kwamba tangu tunakua na kwenda shule, tumekuwa tunaambiwa ni kazi zipi zinazoweza kutupa kipato na zipi hazifai. Kuwa daktari, kuwa mwalimu, kuwa mhandisi au kuwa mhasibu, kisha utapata kazi ya uhakika na kuwa na maisha mazuri. Matokeo yake tumekuwa na watu ambao wanafanya kazi wasizozipenda, hivyo hawatoi thamani kubwa na kipato chao kinakuwa kidogo.
Utajiri wako uko kwenye kile kitu ambacho unapenda kukifanya, maana hiki ndiyo utakuwa tayari kutoa thamani kubwa sana. Kama unapenda kuandika andika, kama unapenda kucheza cheza, chochote unachopenda kufanya, kifanye kwa namna unavyoweza kuongeza thamani kwa wengine na utaweza kutengeneza kipato.

14. Kama umeshapotea, anzia hapo ulipo.
Tunao watu wengi ambao wamepotea kwenye kazi na biashara zao. Wamejikuta kwenye kazi au biashara wasizozipenda, hii ni kwa sababu hawakupata msingi wakati wanaanza. Na sasa wamepata msingi lakini wanaona hawawezi kutoka kwa sababu ya majukumu waliyonayo. Watu hawa wanaweza kuanza kufanya kile wanachopenda kufanya, huku wakiendelea na kazi au biashara zao kwa sasa. Kama upo kwenye kundi hili usiendelee kusubiri, anza sasa. Hakuna siku itafika ambapo utaona uko tayari kwa kila kitu.

15. Hakuna kustaafu.
Ukiangalia watu wote ambao wameweza kufanikiwa sana kifedha, utagundua wanafanya kazi mpaka wakiwa na miaka 70, 80 na hata 90. Hii ni kwa sababu wanajua fedha haina kustaafu, na kingine muhimu ni kwamba wanakuwa hawafanyi kazi, badala yake wanafanya kile wanachopenda kufanya, ambacho wanachukulia ni sehemu ya maisha yao.
Kama unafikiria kustaafu zaidi kuliko unavyofikiria kufanya kazi au biashara yako, upo kwenye njia ambayo siyo sahihi. Pia usiangalie kustaafu kama ndiyo mwanzo wa kuyaishi maisha ya ndoto yako, bali maisha yako yawe ndiyo ndoto yako, kila siku.

16. Huwezi kupata mafanikio ya kifedha kama unataka kufanya vitu vya kawaida.
Kwa kifupi ni kwamba kama hakuna mtu amewahi kukushangaa kwa kile unachofanya, au kustuka au kukuambia unakosea, maana yake hakuna kikubwa unachofanya, unafanya kile ambacho kila mtu anakijua na amekizoea. Ni vigumu sana kupata utajiri kwa kufanya vitu vilivyozoeleka.
Unahitaji kufanya vitu ambavyo siyo vya kawaida, vitu ambavyo havijazoeleka, weka juhudi ambazo hazijazoeleka na utapata matokeo ambayo hayajazoeleka.

17. Usijihukumu kwa matokeo yako ya sasa.
Huwa tuna tabia za kuwahukumu watu kwa matokeo yao ya sasa. Na pia tunajihukumu sisi wenyewe kwa matokeo tunayopata sasa, tunaona pale tulipo ndiyo sehemu yetu na hivyo kuridhika. Hujawahi kujiuliza kwa nini mtu anaweza kufanya kazi miaka 10 au 20 kwa kipato kile kile na madeni kila siku. wanakuwa wamejihukumu na kukubali hukumu zao.
Haijalishi kwa sasa uko wapi, kesho unaweza kuwa bora zaidi ya leo. Na ili kesho uwe bora, ni lazima uchukue hatua leo. Anza kuchukua hatua leo kutengeneza kesho bora. Usikubali sababu yoyote uliyonayo sasa ikuzuie.

18. Sumu kubwa itakayokumaliza kwenye safari ya utajiri.
Ni kuiga. Kwa sababu fulani kafanya kitu fulani akafanikiwa, siyo uhakika kwamba na wewe ukifanya utafanikiwa. Binadamu tunatofautiana, na hakuna mtu yeyote hapa duniani anayefanana na wewe moja kwa moja. Uko hivyo ulivyo wewe tu hapa duniani. Sasa unapojaribu kuiga wengine, unachofanya ni kuzika uwezo wako wa kipekee ulionao. Kamwe kamwe usiige, jua kipi bora kwako a kipi unapendelea kisha weka juhudi zako zote hapo, utafanikiwa.

19. Hakuna mtu ambaye hajawahi kushindwa.
Hadithi utakazosikia kwa wengi ambao hawajafanikiwa ni kwamba nilijaribu nikashindwa. Kama ile wale waliofanikiwa wao walikuwa na njia rahisi, hawakuwahi kushindwa. Sikiliza kila mtu alishawahi kushindwa, tena wale waliofanikiwa ndiyo wameshindwa mara nyingi kuliko wale ambao hawajafanikiwa. Hivyo acha kutumia kushindwa kama kigezo cha wewe kukosa mafanikio. Ukishindwa usikate tamaa, amka na endelea na mapambano.

20. Utajiri au umasikini unaanza na wewe mwenyewe.
Tatizo siyo fedha, tatizo ni mimi mwenyewe, jiambie kauli hii kila mara ambapo unajikuta kwenye changamoto za kifedha, itakusaidia mno kuchukua hatua sahihi. Fikra zako, maamuzi yako na matendo yako yanaathiri sana hali yako ya kifedha. Marafiki unaokaa nao muda mrefu wana mchango kwa hapo ulipo kifedha, kama unabisha waangalie marafiki zako wa karibu, utaona wote mnalingana kwenye swala la fedha. Vipindi vya tv unavyoangalia, magazeti na vitabu unavyosoma vinaathiri hali yako ya kifedha.

Kwa kifupi ni kwamba, kuondoka kwenye changamoto za kifedha, kufikia utajiri na uhuru wa kifedha, akili yako inahusika mno. Anza kuleta mapinduzi kwenye akili yako na linda akili yako isichafuliwe na mitazamo hasi ya kifedha. Utaweza kufanya maamuzi bora na kuweza kufanikiwa

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here